- WAIPINGA PAC,WAJIPANGA KUCHUKUA HATUA
- WATISHA KUSUSIA KIKAO CHAKE OKTOBA 25
Rachel
Balama na Anneth
Kagenda
Chama cha Wananchi (CUF), kinatafakari
hatua za kuchukua pamoja na kumuandikia barua Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda
aweze kuzifunda Kamati za Bunge ili zitambue wajibu wake.Tamko
la CUF linatokana na Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya
Mwenyekiti wake, Bw. Zitto Kabwe, kuvitangazia kiama vyama tisa vya siasa
vinavyopata ruzuku lakini vimeshindwa kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa fedha.
Taarifa
za ukaguzi huo zilipaswa kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa (CUF) Bara, Bw.
Julius Mtatiro, alisema chama hicho kinatekeleza sheria zinazovitaka vyama vya
siasa kupeleka hesabu zao ili zikaguliwe na vyombo maalumu vya Serikali.
Alisema
chama hicho hakihusiki na agizo la Bw. Kabwe aliyedai chama hicho ni miongoni
mwa vyama vinavyopewa ruzuku na kimeshindwa kuwasirisha taarifa za ukaguzi wa fedha
kwa CAG katika kipindi cha miaka minne.
"Pamoja na
kumwandikia Spika barua, CUF haitakutana na Kamati ya PAC, Oktoba 25 mwaka huu
kama alivyodai Bw. Kabwe kwa sababu hatujapewa barua ya wito hivyo hatuwezi
kuitwa kihuni kupitia mitandao ya kijamii.
"Hiki ni chama
cha siasa ambacho kina utaratibu wake, hatuwezi kuitwa katika mkutano kupitia
facebook, twiter, whasapp, google na mitandao mingine ya kijamii, Oktoba 25
hatuendi na gerezani hatuwezi kupelekwa... vielelezo vyote tunavyo na tayari
vimehakikiwa na Msajili wa Vyama," alisema.
Aliongeza kuwa, PAC
imeamua kuligeuza jambo hilo kuwa mtaji wa kisiasa na kusisitiza kuwa, hesabu
ambazo chama hicho hakijawasilisha kwa CAG ni zinazoishia Desemba 31,2012
ambazo wakaguzi wa ndani na nje wamemaliza kuzikagua Julai mwaka huu.
Bw. Mtatiro alisema,
hesabu hizo zitathibitishwa na Kikao cha Kamati ya Utendaji Taifa mwezi huu na
Baraza Kuu la Uongozi Desemba mwaka
huu hivyo hesabu ambazo bado hazijamfikia Msajili ni za mwaka mmoja uliopita.
"Tumesikitishwa
na kauli tulizozisikia kupitia vyombo vya habari kuwa CUF ni miongoni mwa vyama
vilivyoshindwa kuwasilisha hesabu zake kwa CAG miaka minne mfululizo, tunaomba
Watanzania wazipuuze taarifa hizo kwa sababu hazina ukweli wowote,"
alisema Bw. Mtatiro.
Alisema Bw. Kabwe
hana taarifa za kina jinsi CUF ilivyotekeleza wajibu wake na kama Kamati ya
Bunge inafanya kazi zake katika mitandao ya kijamii ni jambo la kufedhehesha."Kamati makini
ya Bunge ni ile inayopokea taarifa kutoka pande zote muhimu, inakutana na wadau
wote, kujua tatizo liko wapi na kuujulisha umma nani amesababisha uzembe,"
alisema. Hivi karibuni Bw.
Zitto alivishutumu vyama vyote vinavyopokea ruzuku na kudai vimeshindwa
kuwasilisha taarifa ya ukaguzi wa hesabu kwa CAG na Msajili wa Vyama vya Siasa.
Hongera Mtatiro kwa ufafanuzi mzuri umeonesha CUF mko safi kiasi gani. Endeleeni na utamaduni huo kwani nchi hii nyinyi ndio tegemeo letu baada ya ccm mafisadi.
ReplyDeleteGreat blog post
ReplyDelete