- WALINZI WASHINDWA KUWABAINI WAHALIFU
Na Kassian
Nyandindi, Ruvuma
Ikulu ndogo anayoishi Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, Senyi Ngaga, imevamiwa na watu wasiofahamika
ambao waliiba kuku waliokuwa bandani.Tukio hilo limetokea usiku wa
Oktoba 2 mwaka huu, ambapo kuku hao walikuwa kwenye banda lililojengwa kwa
matofali.
Wizi huo
umetokea baada ya wezi hao kutoboa ukuta wa banda hilo mbali ya kuwepo ulinzi wa kutosha.
Chanzo chetu cha habari kutoka Jeshi la
Polisi wilayani humo, kilisema askari waliokuwa zamu siku hiyo katika nyumba
hiyo hawakuweza kuwabaini wezi hao.
"Ni tukio ambalo linatuumiza kichwa,
eneo kama hili kuvamiwa na kuvunjwa, uchunguzi
wa kina ufanyike kubaini kwanini wahalifu hawakubainika mapema na
kukamatwa," kilisema chanzo hicho.Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti,
baadhi ya wakazi wa Mbinga walisema ni jambo la kushangaza eneo hilo lenye ulinzi mkali
kuvamiwa na wezi hao kufanikiwa kuiba kuku.
"Mkuu wa Wilaya ni mwakilishi wa Rais
wetu, inakuwaje eneo la Ikulu ndogo analoishi kuvamiwa na wezi wakati vyombo
vya usalama vipo," walihoji wananchi hao.Kamanda wa Polisi mkoani humo, Deusdedith
Nsimeki, alikiri kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa;
"Ni kweli taarifa juu ya kuvamiwa na kuvunjwa banda la
kuku katika Ikulu ndogo nimezipata hivi punde...kuku kadhaa wameibwa. "Idadi yake
sijaipata lakini uchunguzi bado unaendelea ili tuweze kubaini ni nani
aliyehusika na uhalifu huo, hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusika na tukio
hili," alisema.
mh jamani tupeni ukweri
ReplyDeleteikulu inaulinzi mkali ilkuaje watu wakaingia bila walinzi kujua
basi walinzi wote wakae rumande waojiwe