- SIMBA SC YABANWA MKWAKWANI
Mshambuliaji, Hamis Kiiza wa Yanga
jana aliwapa faraja mashabiki wa timu hiyo baada ya kuifungia mabao mawili kati
ya matatu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Rhino Rangers ya
Tabora.
Katika mechi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam mashabiki wa Yanga walionekana kupooza hali
inayoonesha kukata tamaa kutokana na matokeo ya Jumapili baada ya kutoa sare ya
mabao 3-3 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba.
Yanga ilianza kupata bao
dakika ya 12 lililowekwa kimiani na Kiiza, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Simon
Msuva aliyetia krosi katika lango la Rhino.Katika dakika za mwanzo
timu zote zilicheza mchezo wa kuviziana na kuufanya kuwa wa kupooza, huku Yanga
wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.
Dakika ya 43 Yanga
walikosa bao la wazi kupitia kwa Msuva, ambaye alibutua mpira baada ya kupewa
nzuri pasi nzuri na Mrisho Ngassa, ambaye jana alicheza kwa juhudi kubwa
kuhakikisha timu yake inaondoka na ushindi.Kipindi cha pili kilianza
kwa Yanga kuingia na uchu wa kutaka kufunga, ambapo dakika ya 48 nusura, Msuva
angeipatia bao timu hiyo lakini shuti lake likaokolewa
na mabeki wa Rhino.
Kiiza aliikosesha Yanga
bao la wazi, baada ya kubaki na kipa wa Rhino ambaye aliuwahi mpira na
kuudaka..Yanga ilikosa bao lingine dakika ya 70 baada ya Ngassa kufanya kazi
kubwa na kutoa pasi nzuri kwa Kiiza ambaye alipiga shuti kubwa lililotoka nje
ya lango.
Frank Domayo aliipatia
Yanga bao la pili dakika ya 73 baada ya kupokea pasi nzuri ya Ngassa, ambaye
alikuwa akihaha huku na huku kutafuta mabao.Dakika ya 73 Yanga iliongeza bao la
tatu lililowekwa kimiani na Kiiza, baada ya kupewa pande na Ngassa.
Naye Hamis Miraji anaripoti kutoka Tanga
kuwa, Simba jana ilitoka suluhu na Coastal Union katika mechi ya ligi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani.Katika mechi hiyo, Hamis Ndemla wa Simba alikosa bao dakika ya 10 baada
ya kuachia shuti kali lililotoka nje ya lango la Coastal.
Dakika 18 wachezaji wa Simba
walipigiana pasi safi
hadi ndani ya 18 lakini, Hamis Tambwa alishindwa kutumbukiza mpira kimiani,
baada ya kuwa katika nafasi nzuri ya kufunga..Coastal Union nayo ilizinduka dakika ya 19 lakini mshambuliaji wake raia
wa Uganda, Yayo Lutimba
akiwa ndani ya 18 alishindwa kufunga baada ya shuti lake kutoka
nje ya lango. Katika
mechi nyingine iliyochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Prisons
ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi Kagera Sugar
No comments:
Post a Comment