Frank Monyo na Jazila Mrutu
Tanzania
imepokea Uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya
Afrika katika mapambano ya kuzuia na kudhibiti uzagaaji wa silaha haramu
(RECSA), kutoka nchi ya Rwanda.
Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam jana ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Rwanda, Bw.
Mussa Harerimana alikabidhi Uenyekiti huo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Baada ya kupokea uenyekiti huo, Dkt. Nchimbi
alisema nafasi hiyo ataishikilia kwa miaka miwili akiwa na jukumu la kukagua
silaha zote za nchi wanachama na kuzisajili na mikutano yote ya kukabiliana na
uzagaaji wa silaha haramu, itafanyika nchini.
"Mafanikio tuliyopata tangu umoja huo
ulipoanzishwa 2005 ni kusajili silaha zote kwa mfumo wa kisasa... upande wa Tanzania
asilimia 80 ya silaa zimesajiliwa kwa mfumo huo," alisema.
Aliongeza kuwa, mafanikio mengine ni
kuteketeza silaha haramu zilizokamatwa 578 kipindi cha mwaka 2005 hadi hivi
sasa katika nchi wanachama
No comments:
Post a Comment