Jane
Edward, Arusha
Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed
Gharib Bilal, amelitaka Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kujadili suala zima la demokrasia kwenye
chaguzi mbalimbali
Alisema
asilimia kubwa ya wananchi katika jumuiya hiyo, bado hawajui umuhimu wa
kushiriki katika chaguzi hivyo kushindwa kutumia fursa ya demokrasia.
Dkt.
Bilal aliyasema hayo jijini Arusha jana wakati akifungua Mkutano wa 34 wa
Mabunge ya Nchi wanachama wa SADC, unaoendelea mjini humo na kuongeza kuwa,
jumuiya hiyo inapaswa kuliangalia jambo hilo ili kuziepusha nchi zao katika
majanga mbalimbali kama uvunjifu wa amani unaotokea katika matokeo ya Uchaguzi
Mkuu.
Aliongeza
kuwa, jumuiya hiyo ina nafasi kubwa ya kurudisha amani ya nchi ambayo wakati
mwingine inapotea kwa kuwa wananchi hawajui umuhimu wa kupiga kura na kubuni
mbinu mpya za kuwaelimisha wananchi .
"Wananchi
wanapaswa kujua umuhimu wa demokrasia hasa kwenye upigaji kura hivyo lazima
waelimishwe, msikubali amani ya nchi zenu ipotee," alisema Dkt. Bilal.
Alilitaka
jukwaa hilo kuhakikisha linakuwa na hadhi ya
Bunge kamili kama yalivyo mabunge mengine kwani kama
litapata hadhi hiyo, litachangia ongezeko la wingi wa wanawake bungeni na
kusaidia mambo yanayoihusu nchi husika.
Awali
Spika wa Bunge la Tanzania,
Bi. Anne Makinda, alisema Tanzania
bado ina uhitaji wa wabunge kutoka Viti Maalumu ili uwiano wa wabunge wanaume,
wanawake uwe sawa hali ambayo itasaidia mabadiliko ya kiutendaji bungeni.
"Changamoto iliyopo kwa wanawake nchini Tanzania bado
hawajaweza kujitokeza kwa wingi na kushiriki chaguzi mbalimbali kwani bado wana
dhana iliyojengeka kuwa wanawake ni viumbe dhaifu na waoga hivyo kusababisha
wengi wao kubaki nyuma na kuwaona wanaume kuwa ndiyo wanaoweza pekee,"
alisema
No comments:
Post a Comment