Na Amina Athumani
UONGOZI wa Yanga leo utawasilisha
pingamizi la mchezaji wake, Mrisho Ngasa kutokana na adhabu aliyopewa na Kamati
ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).Ngassa
amefungiwa mechi sita na kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa
kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti 17, mwaka huu kati ya Yanga
na Mtibwa.Mchezaji huyo
amepewa adhabu hiyo, baada ya kubainika kwamba ana mikataba katika Klabu za
Simba na Yanga.
Licha ya kufungiwa mchezaji huyo, pia ametakiwa kuilipa Simba sh.
milioni 45 baada ya kuchukua sh. milioni 30 kama
sehemu ya mkataba na fidia ya asilimia 50,ambayo ni sh. milioni
15 ambazo Ngassa ametakiwa kuzilipa ndani ya kipindi cha adhabu yake.Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu
Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema wanatarajia kuwasilisha mapingamizi
matatu TFF kati ya leo na kesho.
A l i s e m a p i n g a m i z i
watakalowasilisha kuhusu mchezaji huyo ni kuhusu adhabu aliyopewa, huku barua
waliyopewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ikiwa haijaainisha
vipengele vya kanuni za kufungiwa kwa mchezaji wao.
"Tulipokea barua kutoka TFF,
ambayo inaelezea tu kwamba mchezaji wetu kafungiwa mechi sita na faini ya sh.
milioni 45, lakini haijaainisha kipengele chochote cha kanuni za ligi
kilichotumika kumuadhibu Ngassa," alisema Mwalusako.Alisema pia ndani ya pingamizi hilo wameelezea kuhusu Simba, kudai kumsajili Ngassa
wakati katika barua yao
waliwasilisha vielelezo ambavyo si halali.
"Kama
ni suala la Ngasa kula pesa za Simba halihusiani na masuala ya usajili
lilitakiwa kujadiliwa baina ya Simba, Yanga na mchezaji mwenyewe na si
kupelekwa TFF," alisema Mwalusako.Ngasa kabla ya kusajiliwa na Yanga
katika msimu uliopita alikuwa akiichezea Simba kwa mkopo akitokea Azam FC
ambayo nayo ilimsajili kutoka kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara
No comments:
Post a Comment