24 August 2013

WIZI WA KUTISHA TPA-KAMATI



Mariam Mziwanda na Anneth Kagenda
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imebaini wizi wa kutisha katika Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na kuhoji kwa kina matumizi ya fedha mbalimbali zikiwamo sh. bilioni 9.1 zinazodaiwa kutumika katika Mkutano Mkuu wa wanachama.Pia kamati hiyo ilihoji matumizi ya sh. bilioni 10 zilizodaiwa kutumika kwa safari za ndani na nje pamoja na sh. bilioni 6.2, zinazodaiwa kutumika kwenye matangazo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Deo Filikunjombe, alisema fedha nyingine sh. bilioni 30, zinazodaiwa kununua mashine za kupakulia mizigo kwa dharura, hazikuwa kwenye mpango na wala hawakupata kibali."Haiingii akilini mnaposema mmetumia sh. bilioni 9 kwenye mkutano...hapa kunamchezo unachezwa, tumemwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), afanye ukaguzi wa fedha hizi ili kubaini ukweli," alisema.
Aliongeza kuwa, kamati hiyo inasikitishwa na ununuzi wa vitu mbalimbali usiofuata utaratibu kama mashine kwani fedha hizo ni nyingi, hivyo kamati haiwezi kuvumilia suala hilo."Kuna sh. bilioni 3 za matibabu kwa wafanyakazi...tumesema wafanyakazi wote wapewe Bima ya Afya, kuna fedha za ununuzi wa mafuta ya gari utakuta wameandika lita 100 kumbe zilitumia lita kama 20.
"Hatupokea ripoti yenu, lazima tujiridhishe kwani tunawapa maelekezo halafu hamtaki kuyafuata pamoja na sheria ya manunuzi, tunajua Waziri anafanya kazi kubwa hivyo hatupaswi kumwangusha," alisema Bw. Filikunjombe.
Katika kikao hicho, uongozi wa TPA haukuwa na majibu mazuri jambo ambalo lilisababisha kamati hiyo kuhoji mambo mbalimbali na kuamua kukataa ripoti hiyo hadi iende kwa CAG kukaguliwa up

No comments:

Post a Comment