Anneth Kagenda na Mariam Mziwanda
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC), imebaini wizi wa mabilioni unaofanywa na Hazina kwa
kutakatisha fedha katika malipo ya halmashauri nchini.Utakatishaji
huo unadaiwa kufanywa kwa kufoji malipo hewa na kuongeza takwimu za fedha
kwenye bajeti za halmashauri
.Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Bw. Rajabu Mbarouk aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza
waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo."Kuna
utoroshaji wa fedha haramu kutoka Hazina kwenda katika halmashauri, kamati hii
imelifanyia uchunguzi jambo hili na tuna mifano ya Halmashauri ya Mbarali
ambayo ilihitaji sh. milioni 70 kwa ajili ya bajeti yake lakini ikapewa sh.
milioni 724.6.
"Halmashauri
ya Wilaya ya Korogwe Mjini (Tanga), walitakatisha sh. milioni 500, Mvomero
(Morogoro), sh. milioni 85 zote kutoka Hazina...hapa kuna mchezo mchafu,"
alisema.Akizungumzia utendaji wa Halmashauri ya Kiteto, alisema
halmashauri hiyo imekuwa na matumizi yasiyo na tija zaidi ya sh. milioni 25 na
kumtaka Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuhakikisha anazingatia sheria na
kuheshimu maamuzi ya Mkurugenzi licha ya
kuwa mwanamke.
"Mwenyekiti
tunakuomba sana
zingatia sheria...huyu mama ni Mkurugenzi, msitumie mila na tamaduni kumuona
hana mamlaka hii nchi inaendeshwa kwa sheria, mila na taratibu zisije kuendesha
nchi mzingatie mamlaka ya Serikali tunalisema hili kwa sababu tumeliona hata
katika majibu yenu," alisema.
Naye Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Bw. Seleman Zedi, alisema halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwamo kushindwa kukusanya sh. milioni 500 kutoka kwa mawakala wa mapato ya
kilimo ambao ni vyama vya ushirika vya kilimo.
Alisema halmashauri hiyo ina ushirikiano mdogo kiutendaji kati
ya halmashauri, madiwani, vyama vya ushirika vya kilimo pamoja na kuwepo
ubadhirifu mkubwa katika nidhamu ya fedha."Kuna mtandao wa ubadhirifu hivyo
kamati imeitaka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),
kufanya ukaguzi wa nyaraka mbalimbali," alisema
No comments:
Post a Comment