Na Rehema Mohamed
MFANYABIASHARA Ahmed Popi (35), jana
alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam,
akikabiliwa na shtaka la kufoji barua na saini ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo
Pinda.
Mbele ya Hakimu
Waliyarwande Lema, wakili wa Serikali Hamisi Saidi, alidai mshtakiwa huyo
alitenda kosa hilo muda na terehe isiyofahamika jijini Dar es Salaam.
Ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa huyo alifoji barua yenye kumbukumbu namba DA
21/2078/01A/142 ya Desemba 3, 2012 kwa lengo la kuonesha ni halisi iliyotolewa,
kusainiwa na Waziri Mkuu Bw. Pinda.Katika shtaka
lingine, ilidaiwa mshtakiwa huyo kwa lengo la kudanganya katika tarehe hizo,
bila ya kupata ruhusa ya mamlaka husika alifoji na kusaini barua hiyo.
Ilidaiwa kuwa,
mshtakiwa alifoji barua hiyo kwa lengo la kumpelekea Islam Mtila na kuonesha
kuwa imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu wakati akijua si kweli.Mshtakiwa
alikana kutende makosa hayo na amerudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini.
Hakimu Lema alimtaka mshtakiwa awe na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya
sh. milioni 10 kila mmoja.
Sharti lingine ni kuwa na mdhamini mmoja kati ya
hao ambaye atasaini hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi
imeahirishwa hadi Septemba 5 mwaka huu, itakapotajwa
No comments:
Post a Comment