Na Damiano
Mkumbo, Singida
.KUNDI la watu
wanaodaiwa kuwa wenye hasira wamechoma moto basi la Kampuni ya Turu la mjini
Singida katika tukio lililotokea katika Kijiji cha Singa Wilaya ya Mkalama Mkoa
wa Singida.Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, tukio hilo
lilitokea juzi Agosti 20, mwaka huu mchana wakati basi hilo likitoka mjini
Singida kwenda Hydom kijijini.
Basi
hilo lilipofika kijijini hapo lilisimamishwa na abiria kutakiwa kushuka pamoja
na kuteremka na mizigo yao.Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana, Kamwela alibaini kuwa
basi hilo nambari T438AHJ lilikuwa likiendeshwa na dereva, Yusufu Lema (36) na
kwamba baada ya kufika kijijini hapo wananchi walilizuia na kuanza kulipiga
mawe.
Alisema
basi hilo lilipasuliwa vioo kwa mawe na kisha kuchomwa moto na kusababisha
hasara inayokadiriwa kufikia sh. milioni 40.Kamanda
Kamwela alisema kuwa uchunguzi ulibaini chanzo cha tukio hilo, mgogoro kati ya
wananchi wa Vijiji vya Singa, Mudida na Nkungi vilivyo kwenye barabara hiyo
kutokana na mtu mmoja, Daudi Songelael (40) kukanyagwa na gari na kusababisha
kifo chake.
Inadaiwa
kuwa basi la Kampuni hiyo T922ALQ lilisababisha kifo cha marehemu Agosti 6,
mwaka huu. Alisema kulikuwa na mvutano kiasi cha kusababisha kuchomwa moto basi
hilo.Alisema
Jeshi la Polisi liliwashauri wamiliki wa Mabasi ya Kampuni ya Turu kusitisha
safari zake kwa muda ili kutafuta suluhisho la mgogoro huo.
Aliongeza
kuwa wamiliki hao walikwenda kijijini hapo Agosti mwezi huu kuomba msamaha bila
kulijulisha Jeshi hilo; na kuanzisha tena safari zake Agosti 20, mwaka huu
wakidhani mgogoro umekwisha.Alisema basi hilo lilipofika kijiji cha Singa
lilikutana na kizuizi na wananchi wakalichoma moto kisha kukimbia
No comments:
Post a Comment