22 August 2013

TANZANIA YATUMA WANAJESHI ANGOLA



.Na Grace Ndossa
WANAJ E SHI 3 5 wa Kamandi ya Jeshi la Anga wamesafiri kuelekea nchini Angola kushiriki zoezi la Blue Zambezi likiwa na lengo la kujenga utayari wa kutoa msaada pindi nchi inapopata majanga.Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ, Meja Erick Komba ilieleza zoezi hilo wanaoshiriki ni nchi wanachama wa SADC katika kujenga utayari
Alisema, kundi hilo linaongozwa na Brigedia Jenerali Azra Wilsoni Ndimgwango ambapo watakaa kwa muda wa siku 12.“Hili ni zoezi la nne kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kwa nchi yetu kushiriki zoezi la SADC, lengo likiwa ni kujenga utayari wa kutoa msaada pindi nchi inapopata majanga, katika usambazaji wa chakula, dawa na vifaa vingine,” alisema.
Pia alisema, katika mkutano huo wakuu wa Majeshi ya Anga kutoka nchi za SADC wataudhuria pamoja na Kamandi ya Jeshi la Anga, Meja Jenerali Joseph Furaha Kapwani.Hata hivyo, Meja Jenerali Hassan Vuai Chema aliwataka wanajeshi hao kuwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na kushirikiana vyema na wenzao katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa. Alisema kuwa, wahusika wote watakapofika Angola wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii, kujifunza na kutoa kile walichonacho ili watu wengine wajifunze kupitia JWTZ na wanatarajia kurejea nchini Septemba 2, mwaka huu

No comments:

Post a Comment