22 August 2013

VIGOGO 23 MANISPAA ILALA MATATANI



Heri Shaban na Rachel Balama
WAKUU wa vitengo na idara wapato 23 wa Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam wamechukuliwa hatua za kinidhamu ambapo wawili kati yao wamesimamishwa kazi kutokana na kutoa vibali vya ujenzi wa ghorofa lililoporomoka katika Mtaa wa Indra Gandhi.

Uamuzi huo ulifikiwa Dar es Salaam jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani waliokutana kujadili mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Fedha na Utawala.Akitangaza uamuzi huo Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Khery Kessy, alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya madiwani kujiridhisha kuwa maofisa hao wanastahili kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kutimiza majukumu yao.
A l i t a j a m a j u k u m u y a o waliyoshindwa kutimiza kuwa ni kushindwa kumshauri na kumsaidia mkurugenzi, kuandaa taarifa vibaya zilizokataliwa na Kamati ya TAMISEMI, kushindwa kutekeleza maazimio ya baraza la madiwani na kamati yake, hususan katika bajeti ya matumizi ya asilimia 60 ya maendeleo na asilimia 40 ya matumizi ya kawaida.
Waliosimamishwa kazi kutokana na ghorofa hilo lililoporomoka ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Majengo, Mhandisi Goodluck Mbanga na Fundi Mchundo, Willbrod Mgyabusi. Mhandisi amesimamishwa kazi kwa kutoa vibali vya ujenzi wa ghorofa 14 badala ya 10.
M w i n g i n e a l i y e a g i z w a achukuliwe hatua za kinidhamu ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dkt. Asha Mahita, kwa kushindwa kumshauri mkurugenzi juu ya utekelezaji wa asilimia 60 wa miradi. Mwingine ni msanifu majengo,Themi Luther, Ofisa Utumishi Mkuu, Geras Pius kwa kushindwa kusimamia ratiba za halmashauri na maofisa wengine.

No comments:

Post a Comment