20 August 2013

WAFANYA BIASHARA KIZIMBANI



 Jazila Mrutu na Hytham Mushi
WAFANYABIASHARA wawili katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Jiji Sokoine Drive kwa kosa la kuuza samaki nje ya soko hilo kinyume na sheria.

Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi mbele ya Hakimu Timoth Lyon alisema, washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 19, mwaka huu katika soko hilo ambapo walikiuka sheria na taratibu za soko hilo.
Magodi aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Seleman Dadi (21) na Khalidi Saidi (49) wakazi wa Kigamboni wilayani Temeke jijini humo.
Hata hivyo, washtakiwa walikiri kosa pia dhamana yao ipo wazi endapo watakuwa na wadhamini wawili na kulipa sh. 50,000 kila mmoja na kesi itatajwa tena Septemba 4, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment