Na Leah Daudi
MAJAMBAZI wawili wameuawa na wananchi wenye hasira baada y a
k ump o r a f e d h a mfanyabiashara, Wiliam Mathias mkazi wa Kijitonyama
jijini Dar es Salaam.Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam, Suleiman Kova alisema tukio hilo lilitokea Agosti 18, mwaka huu, saa
saba mchana maeneo ya Tazara.
Alisema,
majambazi yaliyouawa yalitambulika kwa majina ya Said Hemed (42) mkazi wa
Temeke Mikoroshini na Robert Aloyce (37), mkazi wa Mabibo wilayani Kinondoni
ambapo siku ya tukio yalikuwa na pikipiki mbili aina ya Boxer T 665 CJR huku
nyingine ikiwa imefutika namba.
"Hali hii
inaonesha kuwa, wananchi wana hasira na vitendo wanavyofanyiwa na majambazi,
hivyo waliamua kuwashambulia kwa mawe na kuwaua wahalifu hao," alisema
Kova.
Alisema
majambazi hao, wakati wa tukio, walizingirwa na wananchi waliojitolea ambao
walikuwa wanawafukuzia kwa pikipiki hatimaye kuwakamata.
Kamishna Kova
alisema, baada ya kuzungukwa na wananchi majambazi hao walianza kurusha fedha
hizo walizokuwa wamezipora pamoja na mbinu hizo wananchi waliwatupia mawe kwa
hasira na kuweza kuwajeruhi vibaya.
Aidha, alisema
polisi waliingilia kati na kufanikisha kuwaokoa na pesa taslimu sh. milioni
tano ambazo walifanikiwa kumwibia mfanyabiashara huyo.
Hata hivyo, Kova alisema majambazi hao walifariki njiani wakati
wakipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu kutokana na majeraha makubwa
waliyopata kwa kipigo kutoka kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment