SERIKALI
imesema kuwa ni wakati mwafaka wa kuangalia sheria zilizopo zinazohusu uchafuzi
wa mazingira kutokana na hali halisi kuonesha kuwa asilimia 90 ya uchafu
unaoenda baharini unasababishwa na wananchi, anaripoti Anneth Kagenda.
Hayo yalisema Dar es Salaam jana na Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, John Mngodo wakati akifungua mkutano wa wadau
ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), ambao
unalenga kujadili mambo mbalimbali likiwemo hilo la jinsi ya kuzuia uchafuzi wa
mazingira ya baharini kutokana na vyombo vya baharini na ziwani.
Pia kujadili juu ya sheria na kanuni za uchafuzi wa
mazingira baharini.
Alisema, suala la uchafuzi huo kwa asilimia 90
limekuwa likisababishwa na wananchi hivyo sheria zilizopo zikitumika na zingine
kuibuliwa suala hilo
linaweza kupatiwa ufumbuzi.
“Asilimia 10 ndiyo inayotokana na vyombo vyenyewe
vya majini, mfano meli kuzama na mafuta kumwagika bahari inachafuka, lakini
uchafuzi mkubwa unatokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo kutiririsha maji
machafu,”alisema.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Ahmed Kilima, alisema lengo la semina hiyo ni
kujadili mambo mbalimbali likiwemo watu kufahamu juu ya suala hilo na watu kujua sheria ambazo tayari zipo
wazifahamu na kuzifanyia kazi pamoja na kupata utaalamu
No comments:
Post a Comment