Na Fatuma Rashid
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom,
ambayo ni mdhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara, jana imekabidhi vifaa vya michezo
kwa timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo vikiwa na thamani ya sh. milioni 400.Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Kuu, Saad
Kawemba aliishukuru vodacom kwa kutekeleza majukumu yake yaliyopo katika
mkataba wao na kuzitaka klabu za ligi hiyo kuheshimu chapa ya mdhamini wakati
wote wa mashindano
"Ninatoa wito kwa klabu zote
kutumia kama kanuni zinavyosema, pia viongozi tushirikiane kuhakikisha ligi
inafanikiwa kama inavyotakiwa," alisema. Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha
Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa alisema vifaa hivyo vipo tayari
na anaamini timu zote zimejiandaa vya kutosha na tayari kuingia katika mtanange
wa ligi hiyo."Hii ni ishara kuwa siku hadi
siku, ligi yetu inazidi kuimarika na kuwa na ushindani mkubwa zaidi, hakika
tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya soka hapa nchini," alisema.
Twissa alitoa wito kwa wadau wenye
malengo ya kukuza soka nchini, kujitokeza na kuongeza udhamini katika ligi
hiyo, ili kuleta tija zaidi kwani kwa kufanya hivyo pia itasaidia kukuza vipaji
hapa nchini.Vifaa vilivyokabidhiwa jana ni seti za
jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vikinga ugoko, nguo za
mazoezi na nguo za kawaida na vifaa vingine vinavyohusika katika michezo
No comments:
Post a Comment