Na Amina Athumani
UONGOZI wa Yanga umesema kitendo cha
wachezaji wao wa zamani, Shadrack Nsajigwa na Stephano Mwasika kupeleka barua
ya madai Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) si cha kiungwana ni cha
kuifedhehesha klabu hiyo
.Wachezaji hao waliachwa na Yanga, mara
baada ya kumaliza mikataba yao
mwaka jana, lakini wanaidai Yanga sh.milioni 16.Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu
Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema Yanga haina nia mbaya ya kutaka
kuwadhulumu wachezaji hao kwani wamekuwa wakifanya mawasiliano nao ili wawalipe
fedha zao.
Alisema kati ya sh.milioni 16 wanazodai
wachezaji hao, Nsajigwa anadai sh.milioni 10 na Mwasika sh.milioni 6."Wiki mbili zilizopita tuliwapigia
simu wachezaji hawa, ili tujue jinsi gani tutaweza kuwalipa fedha zao, lakini
hatukuwapata sasa wanataka kuharibu usajili wetu, sisi hatuna nia mbaya na
wachezaji wetu na sidhani kama TFF,
watasitisha usajili wetu kwa sababu hiyo," alisema Mwalusako.
Alisema Yanga imepata taarifa za wachezaji
hao kupeleka barua za madai TFF, hivyo wameamua kutoa taarifa hiyo kutokana na
kwamba huenda shirikisho hilo
linaweza kutoa uamuzi utakaoiathiri klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment