Na Yusuph Mussa, Lushoto
BAADHI ya wadau
wanaoboresha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametaka Serikali itunge kitabu chake,
ambacho viongozi wake watakitumia wakati wa kuapa katika utumishi wao badala ya
kutumia vitabu vitakatifu kama Kurani ama
Biblia.
Walidai
hawaoni mantiki ya kutumia vitabu vya dini wakati utekelezaji wa majukumu yao
hawafuati yale ya Mungu, ikiwemo kushindwa kuzuia ufisadi na wizi unaofanywa na
viongozi hao.
Hayo
waliyasema mwishoni mwa wiki wakati wakichangia Rasimu ya Katiba katika mkutano
wa wananchi wa Jimbo la Mlalo mkoani Tanga, ulioandaliwa na Muungano wa Asasi
za Kiraia Wilaya ya Lushoto (LUSCO) kwa ufadhili wa Shirika la The Foundation
for Civil Society la jijini Dar es Salaam na kufanyika Kituo cha Walimu Mlalo
(TRC).
"Serikali
itafute kitabu chake kwa ajili ya viongozi wake kuapa, lakini wasitumie Biblia
au Kuran kwani hawatekelezi mambo yaliyopo kwenye vitabu hivyo. Kama wangekuwa
wanatekeleza yale yaliyoagizwa kwenye vitabu hivyo tungewakubali, mfano wezi
wametakiwa kukatwa mikono na wazinifu kupigwa mawe hadi kufa.
"Lakini
viongozi hao wanatakiwa kuwa na maadili na kulinda mali ya umma, lakini maagizo
hayo ya Mungu hawayafuati kwanini washike Biblia au Kurani watakapokuwa na
kitabu chao tutataka yale wanayoyatamka basi wayatekeleze kweli, sio kama
wanavyofanya sasa kwenye vitabu vya dini," alisema Hazali Hazali (78),
mkazi wa kijiji cha Mlalo.
OSIE UZAONGA SANA. IYO NKWEI TUPU.
ReplyDelete