26 August 2013

SERIKALI TATU YAIBUA MAZITO LUSHOTO



 Na Yusuph Mussa, Lushoto
BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, wamesema Serikali tatu inaweza kusambaratisha muungano uliopo na vyama vinavyopigia debe mfumo huo vina uchu wa madaraka.Walisema mfumo wa Serikali tatu unaweza kuipasua nchi vipande vipande na kusababisha mateso kwa wanawake, watoto, wazee hivyo maoni ya Katiba Mpya lazima yazingatie umakini.

Us h a u r i h u o ume t o l ewa mwishoni mwa wiki kwenye kikao cha kuchambua na kuboresha Rasimu ya Katiba kilichoandaliwa na Muungano wa Asasi za Kiraia Wilaya ya Lushoto (LUSCO).Kikao hicho kilifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Civil Society la Dar es Salaam, ambacho kilifanyika katika Kijiji cha Mlalo.
Mwenyekiti wa Kumekucha Mwamko SACCOS Ltd, Bi. Hadija Mahande, alisema kama mfumo wa kiutawala utabadilika upo uwezekano mkubwa wa nchi kupasuka vipande."Uroho wa madaraka kwa baadhi ya vyama utatupeleka pabaya, wanaotaka Serikali tatu wanasumbuliwa na tamaa wakiamini ni fursa nzuri kwao ya kupata vyeo," alisema.
Naye Bi. Tatu Jaha, alisema Serikali imeshindwa kutimiza ahadi yake yakuwapa matibabu bure wanawake wajawazito, watoto na wazee hivyo suala hilo linapaswa kuingizwa kwenye katiba ili liweze kutambulika kisheria na kutekelezwa ipasavyo.Bw. Abdi Gila alitaka Mawaziri wachaguliwe kwa kuzingatia taaluma zao ili kuleta ufanisi kwenye utendaji badala ya sasa mwenye taaluma ya udaktari anapelekwa jeshini.
Naye Bi. Margareth Shemhilu, alisema zipo taasisi zinazotetea wanawake, wazee na watoto, lakini hakuna taasisi ya kuwatetea wanaume ambao wengi wao wananyanyasika kwenye jamii."Katiba Mpya iliangalie jambo hili, wapo wanaume ambao wananyanyasika lakini wanaogopa kusema," alisema. Mratibu wa LUSCO, Bw. Rodgers Shelukindo alisema maoni yaliyotolewa na wananchi ni muhimu kwa mustakabali wa nchi na kuongeza kuwa, Katiba Mpya itakuwa bora zaidi kutokana na Serikali kutoa nafasi ya kujadiliwa na asasi za kiraia kupata fursa ya kuandaa midahalo

1 comment:

  1. AWO WAGHOSHI WETOIGHWA NI WAVYEE NI MADASHI AU TIAMBE NI MAPOOGWA.

    ReplyDelete