Na Godfrey Ismaley,Aliyekuwa Lindi
SERIKALI
imeweka wazi kuwa kuanzia leo shughuli ya utandazaji wa bomba la gesi kutoka
Mnazibay mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam unaanza na inatarajia kabla ya
Septemba mwaka huu litakuwa limekamilika
.Utandazaji wa
bomba hilo
lenye urefu wa kilomita 534 unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola za kimarekani
bilioni 1.2, zikiwa ni jitihada za Serikali za kutaka kuongeza uzalishaji wa
umeme nchini ambapo ziada itauzwa ili kukuza pato la taifa.
Waziri wa Nishati
na Madini, Prof. Sospeter Muhongo aliyabainisha hayo mwishoni mwa wiki, baada
ya majumuisho ya ziara maalumu ambayo aliifanya na waandishi wa habari Somanga
Fungu mkoani Lindi ili kujionea namna bomba hizo zitakavyounganishwa leo.
Pia ziara hiyo
ilimjumuisha Balozi wa China
nchini, Lu Yonging ambapo kampuni za China Petroleum Technology &
Development Corporation (CPTDC) na China National Petroleum Corporation (CNPC)
zilishinda zabuni ya kusimamia utandazaji huo wa bomba chini ya usimamizi wa
Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).
Prof. Muhongo alisema kuwa, licha ya
mradi huo wa kutandaza bomba la gesi kuongeza ajira kwa Watanzania, pia baada
ya kukamilika unatarajia kuongeza uzalishaji wa umeme mara mbili ya kiwango cha
sasa ambacho ni zaidi ya Megawati 1,500 nchini kote.
" Tu n a omb a Wa t a n z a n i a
waendelee kuvumilia na kuunga mkono mradi huu ambao tunaamini baada ya
kukamilika kila mmoja ataona manufaa yake, kwa uchumi wa taifa na nishati ya
umeme nchini," alisema Prof. Muhongo.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini,
Lu Yonging alisema Watanzania wana kila sababu ya kujivunia rasilimali zao na
kuunga mkono Serikali ili iweze kuzisimamia kwa manufaa ya taifa lote.
" P i a Ch i n a t ume j i t o l e
a kuwachukua wasomi katika vyuo vikuu nchini Tanzania,
ili waweze kwenda vyuo vikuu nchini China, kupatiwa ujuzi wa namna ya
kusimamia rasilimali gesi asilia kupitia teknolojia ya kisasa. Tutazungumza na
Wizara ya Nishati na Madini ili ituongoze namna ya kuwapata wasomi hao,"
alisema Balozi huyo.
Hata hivyo, gesi asilia ilianza
kugundulika hapa nchini tangu mwaka 1974, kwenye Kisiwa cha Songo Songo mkoani
Lindi huku mwaka 1982 ikigundulika Mnazi
Bay na Ntorya mwaka 2012
mkoani Mtwara.
Aidha, mwaka 2007 iligundulika maeneo
ya Mkuranga mkoani Pwani na mwaka 2008 iligundulika tena eneo la Kiliwani
mkoani Lindi ambapo kwa sasa gesi asilia iliyogundulika katika nchi kavu na
baharini ni zaidi ya futi za ujazo trilioni 41.7.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa, rasilimali gesi asilia inaweza
kutumika katika
maeneo mbalimbali kama kuzalisha umeme,
mbolea, kemikali, nishati viwandani, majumbani na kwenye taasisi na kuendeshea
magari
No comments:
Post a Comment