Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam, jana imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh.
milioni 21 kila mmoja vigogo wanane kati ya watano wa Kampuni ya Development
Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), iliyokuwa ikiendesha na kusimamia
mchezo wa upatu.
Mahakama
hiyo pia imeamuru Serikali kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
ifanye utaratibu wa kurudisha fedha zote za taasisi hiyo zilizothibitika
mahakamani kuwa zilitokana na mchezo huo kwa wanachama waliopanda (fedha) zao
DECI.
Fedha
hizo zinakadiriwa kuwa zaidi ya sh. bilioni 10 zilizokuwa zimehifadhiwa katika
akaunti na benki mbalimbali nchini.
Akisoma
hukumu hiyo kwa niaba ya Hakimu Stuwart Sanga aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo,
Hakimu Aloyce Katemana, alisema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha
mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili washtakiwa na kuwatia hatiani.
Aliwataja
watuhumiwa waliotiwa hatiani kuwa ni Jackson Mtares, Dominick Kigendi, Timotheo
Ole Loitignye na Samwel Sifael Mtares ambapo mshtakiwa Arbogast Kapilimba
aliachiwa huru baada ya mahakama kushindwa kumtia hatiani katika mashtaka yote
mawili yaliyokuwa yakiwakabili.
Hakimu
Katemana alisema, katika shtaka la kwanza washtakiwa hao watatumikia adhabu ya
kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh. milioni 3 kila mmoja.
Shtaka
la pili watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh.milioni
18 kila mmoja na kwamba adhabu zote zitakwenda pamoja.
Alisema
ushahidi ulioletwa mahakamani hapo ulithibitisha kuwa washtakiwa hao
walijihusisha na biashara ya kupokea fedha kutoka kwa wananchi kinyume cha
sheria licha ya BoT kuwakataza kufanya hivyo.
Aliongeza
kuwa, washtakiwa hao ambao ni Wachungaji wa Kanisa la Pentekoste, wakati
wakitoa utetezi wao walikiri kosa hilo na kudai walifanya hivyo wakiwa na lengo
la kuwakwamua waumini wao kutoka katika lindi la umaskini.
Alidai
ilithibitika kuwa DECI haikuwa na biashara nyingine ya kuongeza kipato cha
kuwawezesha kupata faida ya kuwalipa wanaopanda mbegu.
Hata
hivyo, mshtakiwa Mtares na Loitignye, walifanikiwa kulipa faini ya sh. milioni
21 kila mmoja na kunusurika kwenda jela.
Kabla
ya kusomwa hukumu hiyo, wakili wa Serikali Prosper Mwangamila, alisema ni rai
ya upande wa mashtaka kuwa mali, magari, viwanja, nyumba na fedha zote
zilizoshikiliwa katika kesi hiyo zinastahili kutaifishwa.
Alisema
kuendesha biashara ya upatu na kupanda mbegu vyote ni makosa kisheria hivyo
wote hawastahili kufaidika na mali hizo zilizotokana na biashara hiyo.
“Mheshimiwa
hakimu, makosa ambayo watuhumiwa wametiwa hatiani yalikuwa na madhara makubwa
kwa uchumi wa nchi yetu hivyo naomba mahakama yako itoe adhabu kali ili iwe
fundisho kwao na wengine wanaofikiria kufanya biashara hii,” alisema.
Kwa
upande wake, wakili aliyekuwa akiwatetea washtakiwa hao, Hudson Ndusyepo,
aliiomba mahakama hiyo iwape adhabu ndogo wateja wake kwani walitenda kosa hilo
kwa kutojua sheria na walikuwa na nia njema katika uanzishwaji wa biashara
hiyo.
“Kwa
sababu washtakiwa hawana rekodi ya mashtaka huko nyuma, naomba wapewe adhabu
ndogo kwa huruma ya mahakama yako kwani msukumo wa kufanya biashara hii ulikuwa
kuwakomboa waumini wao katika lindi la umaskini,” alisema Bw. Ndusyepo.
Katika kesi ya
msingi, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kuendesha na
kusimamia mradi wa upatu kinyume na kifungu 111A(1,3) cha Sheria ya Kanuni ya
Adhabu Sura ya 16.
Ilidaiwa kuwa, kati
ya mwaka 2007 na Machi 2009, katika Makao Makuu ya DECI, yaliyopo Mabibo
Mwisho, Dar es Salaam, washtakiwa waliendesha na kusimamia mradi wa upatu
katika sehemu tofauti nchini kwa ahadi ya kuwapa wanachama wake fedha zaidi.
Fedha walizokuwa
wakitoa kwa wanachama ni nyingi kuliko mradi waliokuwa wakiufanya.
Shtaka la pili ni
kupokea amana za umma bila kuwa na leseni kinyume na kifungu cha 6(1,2) cha
Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha namba 5 ya mwaka 2006 na kwamba,
washtakiwa wote katika kipindi hicho, wakiwa kwenye Ofisi zao za DECI,
walipokea amana kutoka kwa umma bila leseni.
DECI iliwanufaisha
watu wengi hasa waliojiunga mwanzoni na baadaye kuibuka malumbano kati yao,
Serikali na wanachama waliopinga hatua ya Serikali kusitisha shughuli zake kwa
madai kuwa haiko kihalali.
Kusimamishwa kwa shughuli za DECI, kulitokana na
uamuzi wa BoT kutoa taarifa ya kuw
Mimi jina langu ni Regina Edward nilikuwa ni mmoja wa wanachama wa DECI. Naomba Serikali itufikirie kuturudishia pesa zetu, kwani tulifanya hivyo pia ni katika kujikwamua toka katika hali ngumu ya maisha.
ReplyDeleteSerikali kwa kutoturudishia pesa hizo ambazo tumeambiwa zipo Benki Kuu. Ni kutumaliza kabisaa.
Tunaomba sisi wanachama utaratibu ufuatwe ili tuweze kurudishiwa pesa zetu jamani. Na hasa sisi wanawake wajane tuna watoto wanahitaji kwenda shule na matibabu.
Asante hili ndio ombi langu kwa Serikali. Kwani taarifa za leo zinaonesha Serikali haitorudisha pesa hizo jamani!!!
SERIKALI IPO IMESIKIA.shida utekelezaji tu. pole sana ndugu.
ReplyDelete