KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC), imeunda kamati maalumu ya kufanya ukaguzi wa hesabu
za Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam
kwa madai ya kuwepo ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka, anaripoti
Grace Ndossa na Anneth Kagenda
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Rajabu
Mbarouk, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa
habari.Alisema hivi sasa Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (CAG), anakagua hesabu hizo kwa umakini
zaidi ili kubaini ubadhirifu uliopo.
“Ni mwezi wa pili sasa CAG anakagua
mahesabu ya manispaa hii, pia kuna matumizi mabaya ya madaraka, kuna utata
ambao umejitokeza kwa baadhi ya madiwani wa manispaa hii, wanamtaka Mkurugenzi
aliyesimamishwa kazi Bw. Gabraeli Fuime.
“Madiwani wengine wanamtaka Mkurugenzi
aliyepo sasa hivyo tunashindwa kuelewa mvutano huu wa nini,” alisema.Aliongeza kuwa, baadhi y a wami l i k i
wa ma b a n g o wameilalamikia manispaa hiyo kwa kuwanyanganya na kuwapa
kampuni nyingine hali ambayo imeleta utata.
Bw. Mbarouk alisema manispaa hiyo
imekuwa ikilalamikiwa sana na wananchi pamoja na wabunge hivyo CAG akikamilisha
ukaguzi huo, taarifa itatolewa.Hata hivyo,
alisema mvutano uliopo kwa madiwani hao unaonekana kuna masilahi binafsi kati
yao na Mkurugenzi aliyesimamishwa kazi.
No comments:
Post a Comment