Na Rachel Balama
MAHAKAMA ya Hakimu
Mkazi Kisutu, inatarajia kutoa uamuzi wa dhamana dhidi ya raia wa Bulgaria, Todor Peev Peev (38), Mkazi wa Mbezi Beach
aliyefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na makosa 20 ya wizi wa fedha kwenye
mashine za ATM Agosti 27, mwaka huu
.Hakimu anayesikiliza
kesi hiyo, Waliarwande Lema, alisema kuwa kutokana na mabishano baina ya upande
wa serikali na mawakili wa mshtakiwa, mahakama itatoa uamuzi kama
mshtakiwa atapata dhamana au la kwa mujibu wa sheria.
Mawakili wa mshtakiwa
Aren Mwakyoma na Mathias Kisengu, waliiomba mahakama impatie mteja wao dhamana
kwa kuwa ni raia wa Tanzania
na makazi yake ni jijini Dar es Salaam
na ana watoto wawili ambao wanamtegemea.
Wakili Kisengu,
alisema kuwa pia mshtakiwa wakati anakamatwa aliumizwa na kushonwa nyuzi sita
hivyo akiwa nje ni rahisi sana
kupata matibabu.Awali, ilidaiwa kuwa
Julai 28 na Agosti mosi, mbili, tatu na nne mwaka huu, maeneo mbalimbali Jijini
Dar es Salaam,
mshtakiwa aliiba fedha kwenye akaunti mbalimbali kwenye mashine za ATM zaidi ya
sh.
No comments:
Post a Comment