Na Aneth Kagenda
SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es
Salaam (DAWASCO), limesema uzalishaji maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na
Pwani umepungua kutoka lita 80,000,000 hadi lita 50,000,000 kwa siku.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
DAWASCO makao makuu na ofisa uhusiani Bi. Irene Makene imesema kuwa, hali hiyo
imetokana na pampu mbili za kuchotea maji (pre-lift pump) kwenye Mto Ruvu
kuharibika na hivyo kubaki kwa Pampu mbili zinazofanya kazi kati ya nne
"Kutokana na tatizo hilo DAWASCO
inawaomba radhi wananchi wa Dar es Salaam, Kibaha na Mlanzidi na Pwani kutokana
na kukosa maji katika baadhi ya maeneo hadi hapo huduma zitakaporejea kama
kawaaida," alisema.Bi.Makene alisema kuwa kutokana na hali
hiyo imesababisha uzalishaji kupungua na kuathiri upatikanaji wa maji katika
Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.Alisema kutokana na hitilafu hiyo
mafundi wanaendelea na jitihada za matengenezo ili kuhakikisha upatikanaji wa
maji unarejea katika hali yake ya awali kama kawaida. Alisema maeneo yatakayoathirika ni
Mlandizi, Kibaha, Kibamba, Mbezi, Kimara, Ubungo, Chuo Kikuu, Kibangu,
Riverside, Barabara ya Mandelea, Tabata na Segerea.
No comments:
Post a Comment