Na Mwandishi Maalumu, Zanzibar
SERIKALI imetoa wito
kwa wataalamu wa afya kutoka China waliopo nchini kuangalia pia suala la kinga
ya maradhi mbalimbali badala ya kutilia mkazo zaidi suala la tiba wakati
wanapokuwa nchini. Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza na timu ya watu 25
ya wataalamu wa afya kutoka Jamhuri ya Watu wa China waliomtembelea Ikulu jana.
Timu hiyo ya wataalamu 21 wakiwemo madaktari bingwa iliwasili
nchini mwezi Juni mwaka huu ambayo inatarajiwa kukaa nchini kwa miaka miwili
inatoka Jimbo la Jiangsu China ambako wataalamu wa afya kutoka jimbo hilo wamekuwa
wakija Zanzibar kufanya kazi tangu mwaka 1964.
"Msijishughulishe tu katika kutoa huduma za tiba badala yake
muangalie pia suala la kinga ambalo ni muhimu katika kuimarisha afya za
wananchi," aliwaambia wataalamu hao huku akiwataka kuvitumia vyombo vya
habari vikiwemo vya Serikali kuelimisha jamii juu ya kinga ya maradhi
mbalimbali.
Dkt.Shein amesema timu hiyo ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa pamoja
na kutoa huduma kwa wagonjwa, lakini pia imekuja kutekeleza mpango maalum wa
kusimamia ujenzi wa kituo cha uchunguzi wa maradhi ya njia ya chakula katika
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Unguja na kituo cha kuhudumia wagonjwa waliopata
ajali katika Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba.
"Vituo hivyo ni vipaumbele kwetu kwa kuwa vitapunguza gharama
kwa serikali ya kuwapeleka wagonjwa nje ya Zanzibar kwa matibabu na wakati
mwingine hata kwa uchunguzi," alisema Dkt.Shein.
Alibainisha kuwa hivi sasa wagonjwa wengi wenye matatizo ya njia
ya chakula hulazimika kupelekwa Dar es Salaam au hata nchi za nje; hivyo
kukamilika kwa kituo hicho kutakuwa faraja kwa Serikali na wananchi.
Kwa upande wa kituo cha watu wanaopata ajali huko Pemba alisema ni
muhimu kwa kuwa kumekuwepo na ajali nyingi kisiwani humo hususan katika msimu
wa uchumaji karafuu hivyo kujengwa kwa kituo hicho kumekuja wakati mwafaka.
Wakati huo huo timu ya
wataalamu wa afya kutoka China imesema imejizatiti kuwahudumia wananchi ili
kuhakikisha inatoa mchango wake ipasavyo katika kuimarisha afya nchini.
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa timu hiyo Dk. Lui Ya Ping
wakati alipokuwa akitoa salamu za wataalamu hao kwa Rais.
"Tumejizatiti kufanya kazi kwa bidii kuwahudumia wananchi kwa kuwa
tunaamini kufanya hivyo tutakuwa tumetimiza wajibu wetu uliotuleta humu
nchini," alieleza Dkt. Lu
No comments:
Post a Comment