Na Reuben Kagaruki
SHIRIKA la Usafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam (UDA)
linatarajia kuingiza mabasi 2,000 kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri jijini
ifikapo Juni mwaka 2014.Haya
yalisemwa Dar es Salaam
jana na Mwenyekiti wa Saimon Group, Robert Kisena, wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika ndani
ya UDA kuhusiana na uwekezaji.
Alisema
hadi sasa wameingia ubia na kampuni ya kutengeneza mabasi ya Eicher pamoja na
wasambazaji wa mabasi ya kampuni hiyo ya Africarries kwa ajili ya kufanikisha
uwekezaji huo.
"Tumeanza
mpango mkubwa wa uwekezaji na tumeingia ubia na Eicher na Africarries ambapo
ifikapo Juni, 2014 mabasi 2,000 yatakuwa yamefika nchini na ifikapo Septemba na
Oktoba mabasi mengine 100 itakuwa yamefika na hayo ni mbali na yale
2,000," alisema Kisena.
Alisema
katika awamu ya kwanza walianza na mabasi 30 na sasa mabasi mengine 40 yapo
tayari na yataanza kutoa huduma hivyo kufanya jumla ya mabasi ya UDA kufikia
70. Aliongeza kuwa ifikapo mwaka 2017 UDA itakuwa na mabasi yanayotoa huduma ya
usafiri yapatayo 7,000 na mipango ya kufanikisha uwekezaji huo inaenda vizuri.
"Uwekezaji
huu utakuwa na manufaa kwa wakazi wa Dar
es Salaam...uwekezaji wa UDA nia yake ni kugusa maisha
ya wananchi, tutaleta mabasi ambayo yatasaidia wananchi wa rika zote, wanawake
na wanafunzi," alisema Kisena na kuongeza kuwa;
"Hii sio mipango wa ubabaishaji v i n
g i n e v y o h a t a h a w a wasingekuwepo (maofisa wa Africarriers."
Alisema uwekezaji huo wa mabasi 2,000 utakapoanza zitazalishwa ajira za watu
8,000, hivyo watu wengi wataweza kupata kazi," alisema na kuongeza kuwa;"Nauli za mabasi yetu zitakuwa hazipandi hovyo
hovyo, kwani sisi tupo kwa ajili ya wananchi na hata kama
kutakuwa na hali ya kupanda kwa mafuta, nauli haitakuba inabadilika mara kwa
mara.
Alifafanua
kuwa ununuzi wa mabasi 2,000 ni maandalizi ya kuingia na kutoa huduma kupitia
Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART), kwani mabasi yanayoagizwa
na UDA ni yale yanayokidhi masharti yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwa na
milango miwili ya kutumiwa na abiria.
Aliongeza
kuwa sehemu kubwa ya faida itaelekezwa kwa jamii hasa kwa upande wa elimu na
sekta ya afya. Alibainisha kwamba baada ya UDA kuwa imara hisa zake zitaingizwa
kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE ) ili watu wapate
fursa ya kununua hisa hizo baada ya kutengeneza minzania yake mwakani.
Wakati huo huo, Kisena alisema wao wapo tayari kununua
hisa ndani ya UDA iwapo itafanyika hivyo. "Na sisi tumesikia kwenye vyombo
vya habari kuwa Jiji la Dar es Salaam litauza hisa zake, endapo watafanya hivyo
sisi tutakuwa tayari kuzinunua, lakini hatukatazi mtu mwingine kujitokeza
kuzinunua,"alisisitiza
KWA HILO NAWAPONGEZA SANA.BIGUP.
ReplyDeleteNi jambo jema lakini ni vema pia kuwa makini katika kusimamia mabasi hayo ili yatoe huduma bora zaidi.
ReplyDelete