Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya utafiti madini ya urani yenye
mradi wake ujulikanao kama Mto Mkuju ya Mantra ya Tanzania, imeibuka mshindi
kwa kunyakua tuzo tatu kwenye Tuzo za Rais katika Tasnia ya Uziduaji kwa
makampuni yanayofanya vizuri katika Miradi ya Kijamii na Uwezeshaji (Extractive
Industry Corporate Social Responsibility and Empowerment) kwa mwaka 2012.
Kampuni
hiyo imeshinda tuzo hizo baada ya kuonekana kuchangia miradi mbalimbali katika
sekta ya Elimu, Afya na Ajira na kuibuka mshindi wa pili wa jumla katika
kipengele cha Utafiti.
Akizungumzia
tuzo hizo za kwanza za Rais katika Tasnia ya Uziduaji ikiangaza Miradi ya
Kijamii na Uwezeshaji kwa mwaka 2012, Mkurugenzi Mtendaji wa Mantra Tanzania,
Asa Mwaipopo, alisema Tuzo hizo ni uthibitisho mkubwa cha mipango mizuri na
utekelezaji wa miradi bora ya kijamii waliyonayo.
"Kutambulika
huku itakuwa chachu kwa kampuni yetu kuongeza nguvu zaidi katika miradi
mbalimbali ya kijamii," alisema
Tuzo hizo
zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete, ziliandaliwa na Wizara ya Nishati na
Madini kupitia Jukwaa la Wadau wa Tasnia ya Uziduaji (Extractive Industries
Stakeholders Forum - EISF).
Katika tuzo hizo,
kampuli zilizoshindanishwa katika tasnia hii ya uziduaji ziligawanywa katika
makundi manne. Kulikuwa na kampuni kubwa ya uchimbaji wa madini, kampuni ya
kati ya uchimbaji wa madini, kampuni za mafuta na gesi pamoja na kampuni za
utafiti wa mafuta, madini na gesi.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliachim Maswi, Kaimu Kamishna wa madini
Ally Samaje, Balozi wa Canada
nchini Tanzania Alexandre Leveque, na baadhi ya wabunge na wadau mbalimbali
kutoka katika tasnia ya uziduaji.
No comments:
Post a Comment