HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam
imetangaza kuwa mchakato wa kujenga vituo vya mabasi yaendayo mikoani na nchi
jirani katika maeneo ya Mbezi Luis, Boko Basihaya na Kongowe unaendelea vyema, anaripoti
Hytham Mushi.
Mkuu wa Kitengo
cha Uhifandi na Uhusiano wa Jiji, Gaston Makwembe aliyasema hayo jana Dar es
Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Idara ya Habari
(Maelezo).
Alisema kuwa,
ujenzi wa vituo hivyo ni utekelezaji wa mipango ya jiji ya kuimarisha huduma ya
usafiri jijini humo.
Alisema, Kituo
cha Mbezi Luis kitahudumia wasafiri wa Kanda ya Kati na Nyanda za Juu wakati
kituo cha Boko Basihaya kitatoa huduma kwa wasafiri wa Kanda ya Kaskazini huku
Kanda ya Kusini Halmashauri ya Jiji itajenga Kituo cha mabasi Kongowe.
“Kutokana na upembuzi
yakinifu wa awali, ujenzi wa vituo hivyo unakadiriwa kugharimu kiasi cha sh.
bilioni 40 kwa kila kimoja, pia tunabaini vyanzo vya fedha na kuangalia
uwezekano wa kuzishirikisha taasisi mbalimbali za fedha na wawekezaji
wanaoonyesha nia ya kushirikiana na halmashauri ya jiji,” alisema.
Alisema, katika kipindi cha maandalizi ya ujenzi wa
vituo hivyo, Kituo cha Mabasi Ubungo (UBT) kitaendelea kutoa huduma kwa
wasafiri waendao mikoani na nchi jirani na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa
vituo hivyo, Kituo cha Ubungo kitakuwa kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi (DART
No comments:
Post a Comment