Na Elizabeth Mayemba
UONGOZI wa Klabu ya Simba unatarajia kuwatambulisha rasmi
wachezaji wake wa kimataifa kutoka Burundi,
katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Mafunzo ya Zanzibar
itakayochezwa Jumapili ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni
mshambuliaji Amisi Tambwe na beki Gilbert Kaze ambao tangu wasajiliwe na timu yao mpya ya Simba
mashabiki wao hawakupata nafasi ya kuwashuhudia.Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala
alisema, pamoja na wachezaji hao kuonekana kesho mjini Arusha wakati timu hiyo
ikicheza na JKT Oljoro katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mashabiki wa Dar es Salaam wao
watawaona wachezaji hao Jumapili.
“Siku ya Simba
Day wachezaji hawa hawakuonekana mbele ya mashabiki wetu, hivyo Jumapili
tutatumia nafasi hiyo kuwatambulisha rasmi kwa mashabiki na wanachama wa
Simba,” alisema Mtawala.Alisema kwa kuwa
vibali vya kufanya kazi nchini vya wachezaji hao vimepatikana, hivyo ni nafasi
nzuri kwa wana-Simba kuona burudani kutoka kwa wachezaji hao ambao walikuwa
wakisubiriwa kwa hamu kubwa.
Mwenyekiti wa Simba Aden Rage
alifanikiwa kupata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) za wachezaji hao baada
ya juzi kupanda ndege hadi Burundi
kwa ajili ya kushughulikia suala hilo.Rage alisema alilazimika kuingilia kati suala hilo kwa sababu lilihusu
baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na ukweli kwamba
viongozi wa Vital’O, klabu waliyotoka
wachezaji hao hawakuwa mjini na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu Simba. S i m b a walianza L i g i Kuu kwa kulazimishwa sare ya
mabao 2-2 na Rhino Rangers mechi i l i y o c h e zwa Uwanja wa Ally Hassan
Mwinyi mjini Tabora.
No comments:
Post a Comment