- ADAIWA KUTOA AMRI KWA VIGOGO WA POLISI
- POLISI KUWEKA HADHARANI UTAPELI WAKE
Na
Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kumnasa Bw. Alquine Masubo (42), akidaiwa
kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa, siri nzito juu ya vitendo vinavyodaiwa
kufanywa na mtuhumiwa huyo, sasa zimeanza kufichuka.
Habari
na picha zilizochapishwa na gazeti hili juu ya tukio la kukamatwa Bw. Masubo,
ziliibua maswali mengi kwa baadhi ya wasomaji ambao baadhi yao walipiga simu katika chumba cha habari na
kudai wao ni miongoni mwa waliotapeliwa na mtuhumiwa huyo.
Mkazi
mmoja wa Dar es Salaam (jina tunalihifadhi), alisema mtuhumiwa ambaye huwa na
kawaida ya kushirikiana na mke wa kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi, amewahi
kumbambikia kesi ya utapeli na kujitambulisha kwake kuwa yeye ni Ofisa wa Idara
ya Usalama wa Taifa.
Alisema, baada ya kukamatwa na kufikishwa kituo kimoja cha
polisi Dar es Salaam, mtuhumiwa alitoa agizo kwa Kamishna Msaidizi wa jeshi hilo (sasa ni mstaafu),
atoe amri kwa RCO (Mkuu wa Upepelezi), aweze kukaguliwa nyumbani kwake
"Walipokwenda
nyumbani kwangu na kukosa nyaraka ambazo walikuwa wakizitafuta, walichukua vitu
mbalimbali ndani kwangu ambavyo ni pamoja na kitanda, godoro, sofa, kabati,
friji, DVD, televisheni, redio kubwa na vingine vingi.
"Kabla
hawajachukua vitu hivyo, alimwambia mdogo wangu ampe sh. milioni tatu ili
nisichukuliwe vitu vyangu, alipewa sh. milioni moja, lakini bado alitoa amri
vitu vyangu vibebwe licha ya kutoa risiti ya kila kitu walichochukua.
"Pia
alimtaka mdogo wangu ampe pesa ili niweze kupewa dhamana mahakamani, kesi
niliyobambikiwa dhamana yake ilikuwa wazi... aliwaambia waendesha mashtaka kuwa
yeye ni Ofisa Usalama kutoka Ikulu, ambayo imemtuma ili nisipewe dhamana,"
alidai mkazi huyo.
Aliongeza kuwa, kutokana na agizo hilo alikaa gerezani
miezi mitatu, lakini alisaidiwa kupewa dhamana kutokana na juhudi za dada yake
ambaye ni karani wa mahakama (bila kumtaja jina wala mahakama anayoifanyia kazi
jijini humo).
Mkazi huyo aliongeza kuwa, wakati akiwa
mahabusu katika kituo kimoja cha polisi Dar es Salaam, mtuhumiwa (Masubo)
alikwenda kituoni hapo na kumtaka atoe maelezo anayotaka yeye na asipofanya
hivyo, atambambikia kesi kubwa zaidi.
"Nilikataa kuandika maelezo anayotaka yeye, wakati huo ndugu zangu
walikuwa nje, mtuhumiwa aliwafuata na kuwaambia sitaki
Akizungumza na
gazeti hili kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Kamanda wa kanda hiyo,
Kamishna Suleiman Kova, alisema mbali ya tukio hilo,
jeshi hilo pia
litazungumzia mambo mengine makubwa waliyoyabaini.
"Mkutano
wangu wa kesho (leo) na waandishi wa habari, nitazungumzia tukio hilo, pia kuna mambo mengine makubwa ambayo tunatarajia
kuyazungumzia si hilo
tu," alisema.
Aliongeza kuwa,
tayari kuna kikosi maalumu cha polisi ambacho kinaendelea na uchunguzi wa tukio
hilo.
Mlipuko huo
ulitokea juzi ambapo bomu hilo
linadaiwa kutengenezwa kwa chupa na kujazwa petroli ambapo madhabahu, gari la
mchungaji vinadaiwa kuungua.
Mchungaji wa
usharika huo, Noah Kipungu juzi alisema chupa za bia zilizojazwa mafuta hayo
zikiwa zimezibwa na mifuniko iliyotobolewa tundu, ziliwashwa moto ili kuchochea
mlipuko huo.
Alisema katika
tukio hilo,
hakuna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa zaidi ya watu kukumbwa na taharuki.
kutoa maelezo hivyo atanipoteza na
sitaonekana tena uraiani.
"Nd u g u z a n g u wa l i k u j a
kunibembeleza nibadilishe maelezo na kuandika aliyotaka mtuhumiwa, lakini
nilikataa....baada ya kusoma habari za mtuhumiwa katika gazeti lenu (Majira),
Ofisa mmoja wa polisi ambaye alihusika kumkamata Bw. Masubo, alinipigia simu na
kunieleza usumbufu aliopata akitakiwa kumuachia mtuhumiwa.
Aliongeza kuwa, inawezekana mtuhumiwa
amewatapeli watu wengi hivyo, Agosti 28, mwaka huu atakwenda Kituo cha Polisi
Kati ili aweze kufikisha malalamiko yake.
"Kwa sasa nipo Tanga.. kwa shughuli
zangu za kibiashara, narudi Dar es
Salaam keshokutwa (kesho), Jumatano nakwenda kutoa
malalamiko yangu dhidi ya huyo jamaa Kituo cha Polisi Kati," alidai.
Kamanda Kova
Kutokana na tuhuma hizo, gazeti hili
lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman
Kova, kama kuna baadhi ya watu waliojitokeza
kulalamikia utapeli wowote waliofanyiwa na mtuhumiwa.
Katika majibu yake, Kamishna Ko v a a l
i s ema j e s h i h i l o litazungumzia sakata la ofisa huyo leo saa saba mchana
na kama kuna maswali yaulizwe katika mkutano huo.
"Wiki iliyopita nilizungumzia
suala hili, katika kituo kimoja cha redio, lakini kama
kuna maswali yoyote, mje kesho saa saba (leo) katika mkutano wangu na waandishi
wa habari, nitazungumzia sakata zima la huyo Ofisa Usalama feki," alisema.
Akizungumzia juu ya mtuhumiwa kudaiwa
kushirikiana na baadhi ya vigogo ndani ya jeshi hilo
alisema; "Sifahamu lolote kuhusu hilo
ila nalipokea, tutaanza kulifanyia kazi," alisema
AJIRA NDIO TATIZO SASA WATU WANABUNI AJIRA.
ReplyDelete