Na Hamisi Nasiri, Nachingwea
TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi
imewafikisha mahakamani viongozi wawili wa chama cha msingi cha ushirika cha
Naipanga wilayani humo kwa makosa ya kula njama ya kutenda kosa la
rushwa,matumizi mabaya ya nyaraka na ubadhirifu wa fedha za chama hicho.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wi l
aya , Co sma s Heme l e, Mwendesha mashtaka wa taasisi hiyo hiyo, Dismas
Muganyizi aliwataja viongozi hao kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Salumu Tewa
na mwandishi wa chama hicho, Mustafa Kanteu.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja kwa kukusudia wanatuhumiwa mnamo
Juni 30 mwaka huu kwa kutumia risiti yenye namba 027859 walijipatia kiasi cha
shilingi 491,000 fedha za chama cha msingi cha Naipanga.
Muganyizi alieleza mahakamani hapo kuwa viongoz i hao walijipatia
kiasi hicho cha fedha kwa madai ya kununulia kioo cha gari la mizigo ya chama
hicho jambo ambalo lilibainika kuwa halikuwa la kweli ambapo kwa mujibu wa
vifungu 22,28,32(1) namba 11 ya mwaka 2007 vya sheria ya kuzuia na kupambana na
rushwa ni kosa. Mtuhumiwa Salumu
Tewa yupo nje kwa dhamana huku Mustafa Kanteu akirudishwa rumande baada ya
kukosa udhamini hadi Agosti 29 kesi hiyo itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment