Na Darlin Said
TAASISI ya Wanafunzi wa Vyuo Vya Elimu ya Juu (TAHLISO) imelaani vikali
matukio yaliyojitokeza katika mkutano wa baadhi ya viongozi wa Serikali za
Wanafunzi wa Vyuo vya elimu ya juu hapa nchini uliofanyika mkoani Morogoro hivi
karibuni na kudai kuwa ni ulikuwa kinyume na maadili.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Mtendaji wa
TAHLISO, Donati Salla alisema mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya kupambana
na maadui watatu ambao ni Ujinga, Maradhi na Umaskini (FPID) na sio TAHLISO
kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Alisema
katika mkutano huo mbali na mambo yaliyozungumzwa kubwa lililokuchukua uzito
mkubwa ni suala la ni nani awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo
Mwaka 2015.
Kutokana
na hali hiyo Salla alisema TAHLISO inasikitishwa na tukio hilo kwani Serikali
yao inashughulika na masuala ya wanafunzi na ubora wa taaluma itolewayo katika
chuo husika na masuala mengine ya kitaifa lakini si ushabiki wa kisiasa au
kutetea kundi au maslahi ya watu fulani.
"Jukumu
la vyama vya siasa vilivyosajiliwa na kutambulika kiserikali kukaa na kuchagua
au kuteua wajumbe wanaogombea nafasi mbalimbali za kisiasa iwe katika chama,
serikali au vinginevyo lakini hilo siyo jukumu la wanafunzi wa vyuo vya elimu
ya juu,"alisema Salla.
Mbali
na hilo alisema vikao vyote vinavyohusu mjumuiko wa Serikali za wanafunzi
vinapaswa kuitishwa na kuratibiwa na TAHLISO na siyo taasisi nyingine yoyote.
Hivyo TAHLISO inatoa onyo kali
kwa viongozi wa Serikali za Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambao
walishiriki kwenye mkutano huo na kuwataka kutorudia tena na kuwataka kutimiza
jukumu lao la kusoma na kujifunza taaluma zao kwa taratibu zilizoainishwa na
chuo husika.
No comments:
Post a Comment