Na
Moses Mabula, Nzega
MKUU wa Wilaya ya Nzega, mkoani
Tabora, Bituni Msangi, anatarajia kuwaongoza baadhi ya madiwani kwenda kwa
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kulalamikia mpango wa Wilaya hiyo kucheleweshwa
kuwa Halmashauri ya Mji.
Kikao cha Baraza la Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo, kilichokaa hivi karibuni kilimteua Msangi na baadhi
ya wajumbe kwenda kumuona Bw. Pinda ili aweze kulitolea ufafanuzi.
M a d i w a n i h a o
wanashangazwa na mpango huo kuchelewa mbali ya taratibu zote za kuanzishwa
kwake kukamilika.
Walisema utekelezwaji mpango huo
unachukua muda mrefu wakati Wilaya nyingine kama
Tarime, mkoani Mara, tayari imetangazwa kuwa Halmashauri ya Mji.
A k i j i b u h o j a h i y o ,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bw. Ab d u l a h ama n Md eme ,
alisema kuwa ofisi yake tayari iliwasilisha maelekezo yaote muhimu kutoka Ofisi
ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), likiwemo suala
la kuongeza kata na mipaka.
K w a u p a n d e w a k e , Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Bw. Patrik
Mbozu, alisema hatua ya kumteua Msangi kwenda kumuona Bw. Pinda anaiunga mkon
No comments:
Post a Comment