Na Anneth Kagenda
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, leo litazungumzia tukio
la mlipuko unaodaiwa ni bomu ambalo lilirushwa kwenye Kanisa la Kiinjili
Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Segerea, Dar es Salaam
Akizungumza na
gazeti hili kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Kamanda wa kanda hiyo,
Kamishna Suleiman Kova, alisema mbali ya tukio hilo,
jeshi hilo pia
litazungumzia mambo mengine makubwa waliyoyabaini.
"Mkutano
wangu wa kesho (leo) na waandishi wa habari, nitazungumzia tukio hilo, pia kuna mambo mengine makubwa ambayo tunatarajia
kuyazungumzia si hilo
tu," alisema.
Aliongeza kuwa,
tayari kuna kikosi maalumu cha polisi ambacho kinaendelea na uchunguzi wa tukio
hilo.
Mlipuko huo
ulitokea juzi ambapo bomu hilo
linadaiwa kutengenezwa kwa chupa na kujazwa petroli ambapo madhabahu, gari la
mchungaji vinadaiwa kuungua.
Mchungaji wa
usharika huo, Noah Kipungu juzi alisema chupa za bia zilizojazwa mafuta hayo
zikiwa zimezibwa na mifuniko iliyotobolewa tundu, ziliwashwa moto ili kuchochea
mlipuko huo.
Alisema katika tukio hilo, hakuna mtu
aliyekufa wala kujeruhiwa zaidi ya watu kukumbwa na taharuki
HICHO NI KITENDO CHA KISHENZI. ILA MUNGU YU MWEMA ATAJIBU.
ReplyDeleteKWELI MUNGU ATAJABU NA OLE KWA ALIYEFANYA KITENDO HIKI KIOVU MAANA AMEJITAFUTIA LAANA
ReplyDelete