Na Steven William,
Muheza
IMEELEZWA kwamba hadi ifikapo mwaka
2015 huduma ya nishati ya umeme itakuwa imesambazwa vijijini kwa asilimia 30
nchi nzima kutoka asilimia 21ambayo ipo hivi sasa.Hayo yalisemwa
na Mtaalam mshauri na mkufunzi, Mzumbe Mu s a k u t o k a Wa k a l a wa
kusambaza nishati vijijini ( REA) katika mafunzo ya kuhudumia na kurekebisha
mifumo ya umeme wa jua ambayo yamefanyika wilayani Muheza.
Alisema kuwa
wakati mpango huo wa usambazaji huduma ya nishati inaanza kupitia REA umeme
ulikuwa umesambazwa asilimia 10 nchini lakini baada ya mradi huo kuanza
imefikia asilimi 21 sasa kutoka asilimia 10.Musa alisema
kuwa mwanzo wa usambazaji umeme vijijini ilikuwa asilimia mbili kitu ambacho
tofauti na sasa asilimia 21 toka REA waingie kusambaza nishati hiyo vijijini.
Musa alisema
kuwa baada ya kutoa mafunzo hayo ya ufungaji vifaa vya umeme jua kwa vijana 35
watakwenda kufanya kazi kwa vitendo kwa kufunga katika Zahanati tatu wilayani
Muheza.Al i t o a c h
a n g amo t o kwa halmashauri ya Wilaya ya Muheza pindi nishati hiyo
itakapofungwa watenge bajeti ya kufanya matengenezo kama vile taa zikiungua na
kununua betri.
Hata hivyo
Ofisa Maendeleo ya Jamii wilayani Muheza, Vije Mfaume alimhakikishia mkufunzi
huyo kuwa watatenga fedha za kuendelea kuzihudumia sola hizo pindi
zikiharibika.Nae Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Amiri Kiroboto alishukuru huduma hiyo
kufika wilayani humo.
Kwa upande wake
mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Muheza, Paul Moshi ambae alimwakilisha Mkuu
wa wilaya hiyo, Subira Mgalu akifungua mafunzo hayo ya siku nane alisema kuwa
mafunzo hayo yatafanikisha kupata umeme katika vijiji vya Muheza.Alisema kuwa ifikapo mwaka 2015 wanataka kuona
wilaya ya Muheza vijiji vyote vinakuwa na nishati ili kuendeleza huduma za
jamii na kuwahamasisha wananchi vijijini kutumia nishati hiyo
No comments:
Post a Comment