Na Heri Shaaban
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajia
kuanza kuwakopesha mikopo ya riba nafuu wanachama wake walio hai ili
kuwawezesha kuwa na maendeleo na kukuza mitaji yao ya biashara.Hayo yalisemwa
Dar es Salaam jana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa CCM, JeremiahWambura wakati wa mkutano wa wanachama wa CCM katika Mtaa wa Kifuru Kata
Kinyerezi
. Wambura alisema mikakati hiyo ya kutoa
mikopo inatarajia kuanza hivi karibuni ambapo CCM inafanya mazungumzo na
wafadhili mbalimbali watakaosimamia utoaji wa mikopo hiyo.
Alisema kuwa masharti ya kujiunga
katika mikopo hiyo ni lazima awe mwanachama na mwenye kadi ya CCM ambapo ada ya
kujiunga ni sh.20,000 ambapo mpango huu unatarajia kusambaa nchi nzima."Mikopo hii tunatoa kwa wanachama
wetu waweze kujishughulisha katika biashara na kukuza mitaji yao na kuondokana
na umaskini," alisema Wambura.
Alisema CCM
imethubutu na inaweza na kwa sasa inasonga mbele na ambapo katika Afrika ni
nchi ya pili kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hivyo juhudi zaidi
zinaendelea ili kuwawezesha Watanzania kuwa na maendeleo
No comments:
Post a Comment