. Na Severin Blasio,
Morogoro
WATU
wasiofahamika wame h u j umu kwa kung'oa na kupasua mabomba ya maji katika
kijiji cha Pangawe kilichopo Kata ya Mkambarani wilayani Morogoro.Kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa watumiaji maji wa Mkambarani, Ruben Chabaliko hujuma hiyo
inadaiwa kuanza Julai 15 zimeharibu bomba kuu lenye ukubwa wa inchi 22
zinadaiwa kusababishwa wananchi ambao hawaungi mkono huduma hiyo ya maji
kugharimiwa kama ilivyopendekezwa na Jumuia ya watumiaji maji katika Kijiji cha
Mkambarani
"Hujuma hizo zilianza tangu Julai
15 kwa kulipasua bomba kuu lenye ukubwa wa nchi 22 linalotoka milima ya Uluguru
katika maeneo ya mlima Ng'alo-Kiloka na baadae kurudiwa tena Julai 17 katika
eneo la mashamba ya mkonge Pangawe lakini hali hiyo ikarudia tena Agosti 20
maeneo ya Mkongeni kwenda Mkambarani"alifafanua Chabaliko.
Akitoa ufafanuzi wake kwa waandishi wa
habari, Chabaliko alisema wananchi wanasikitishwa na Serikali kushindwa kutoa
ushirikiano katika kulikabili suala hilo.Kutokana na hujuma hiyo Chabaliko
alisema wananchi sasa wanapata usumbufu wa maji na kufanya baadhi ya taasisi na
makampuni ikiwemo Gereza la Mtego wa Simba na Kiwanda cha Tumbaku cha Alliance
One na Zahanati kukosa huduma hiyo.
Hata hivyo tayari uharibifu huo
umeigharimu ofisi ya watumia maji katika Kijiji cha Mkambarani kupata hasara ya
zaidi ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya matengenezo ili kunusuru wakazi
wasipate adha ya kukosa maji.Alipotafutwa kujibu madai ya kuwapuuza
wananchi juu ya tukio hilo Mkuu wa wilaya hiyo, Said Amanzi alisema yeye
hahusiki na matatizo hayo huku akiwataka waandishi kuonana na Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, Julius Madiga na viongozi wa Serikali za vijiji
No comments:
Post a Comment