Ramadhani Libenanga na Rehema
Mohamed
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda, j a n a ame p a n d i s h w a kizimbati katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Morogoro, chini ya ulinzi
mkali wa askari polisi baadhi yao wakiwa na mbwa.
Jeshi
la Polisi lilitumia helikopta yao
kumsafirisha Shekhe Ponda hadi katika Uwanja wa Ndege wa Gofu, mkoani humo.
Katika kesi hiyo, Shekhe Ponda alisomewa mashtaka matatu na wakili wa Serikali,
Bw. Bernard Kongola mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Bw. Richard
Kabate.
Bw.
Kongola alidai Agosti 10 mwaka huu, katika eneo la Kiwanja cha Ndege Manispaa
ya Morogoro, Shekhe Ponda aliwaambia Waislamu kuwa; “Msikubali uundwaji wa
kamati za ulinzi na usalama za misikiti.
“Kamati
hizo zimeundwa na Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA), ambao ni vibaraka wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Serikali.
“Kama
watajitokeza kwenu watu na kujitambulisha kama wao kamati za ulinzi na usalama
za misikiti, fungeni milango na madirisha ya msikiti muwapige,” alifafanua Bw.
Kongola.
Aliongeza
kuwa, kauli hiyo iliumiza imani za watu wengine jambo ambalo ni kinyume cha
agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, iliyotolewa na Hakimu
Victoria Nongwa, Mei 9 mwaka huu.
Alisema
Hakimu Nongwa alimtaka Shekhe Ponda kuhubiri amani ndani ya mwaka mmoja hivyo
kauli aliyoisema ni kinyume na kifungu cha Sheria namba 124 cha mwaka 2002.
Shekhe
Ponda alilikana shtaka hilo ambapo Bw. Kongola alisema, katika shtaka la pili
Agosti 10 mwaka huu, katika eneo la Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro,
mkoani humo, aliwaambia Waislamu Serikali ilipeleka jeshi Mtwara kuzuia vurugu
zilizotokana na gesi.
Alidai
Shekhe Ponda katika vurugu hizo jeshi lilifanya mauaji, kuwabaka na kuwatesa
wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa Mkoa huo ni Waislamu, lakini
Serikali haikufanya hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu
asipatiwe kipande cha ardhi ya uwindaji na kudai ni mali yao.
Aliongeza
kuwa, Shekhe Ponda alidai asilimia 90 ya wakazi wa Loliondo ni Wakristo, Bw.
Kongola alisema maneno hayo yaliumiza imani za watu wengine jambo ambalo ni
kinyume na kifungu cha sheria 129 cha mwaka 2002, shitaka ambalo lilikataliwa
na mshtakiwa Shekhe Ponda.
Katika shtaka la tatu
ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Agosti 10 mwaka huu, eneo la Kiwanja cha Ndege
Manispaa ya Morogoro, mshtakiwa huyo alidaiwa kuwalisha maneno ya uwongo
Waislamu juu ya sakata la Mtwara, Loliondo.
Alisema kauli hiyo ni
kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka
2002, shtaka ambalo Shekhe Ponda alikana.
S h e k h e P o n d a
a l i k uwa akitetetewa na wakili Ignas Pungu na Bantalomeo Tarimo wakati
upande wa Serikali alikuwepo Bw. Kongola, Gloria Rwakibalila na Asnab Mhando.
Baada ya kusomewa
mashtaka hayo, Bw. Kongola aliiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi
umekamilika hivyo iliahirishwa hadi Septemba 2 mwaka huu.
Upande wa utetezi
uliomba kesi hiyo isikilizwe Agosti 26 mwaka huu ambapo Hakimu Kabate
alilazimika kuahirisha kesi kwa muda na baada ya kurudi, aliipanga Agosti 28
mwaka huu, kwa ajili ya kusikilizwa.
Mawakili wa utetezi
walisema, sababu za kuomba isikilizwe mapema ni ugonjwa wa mteja wao hivyo
anahitaji kupatiwa matibabu ya mara kwa mara na uangalizi wa karibu.
Ulinzi uliimarishwa
katika eneo la mahakama ambapo msafara wake wakati akipelekwa mahakamani
ulikuwa na magari matatu ya Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Shekhe Ponda
alirudishwa Uwanja wa Ndege wa Gofu saa sita mchana na kupanda helikopta ya polisi
iliyomrudisha
hadi Dar es Salaam na
kupelekwa mahabusu ya Segerea.
Ponda afutiwa mashtaka
Ka t i k a h a t u a
n y i n g i n e , Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amemfutia Shekhe Ponda
mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
DPP aliwasilisha hati
ya kutokuwa na haja ya kuendelea na kesi dhidi ya mshtakiwa huyo mahakamani
hapo jana.
Mshakiwa huyo alikuwa
akikabiliwa na kesi hiyo mbele ya Hakimu Helleni Liwa wa mahakama hiyo ambapo
jana asubuhi Shekhe Ponda alifikishwa mahakamani hapo.
Mbele ya Hakimu Liwa,
wakili wa Serikali Tumaini Kweka aliieleza mahakama hiyo kuwa, DPP amewasilisha
mahakamani hapo hati ya kutoendelea na mashtaka dhidi ya mshtakiwa hivyo
anaomba kumfutia mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Hakimu Liwa
alikubaliana na ombi hilo na kumfutia mashtaka mshtakiwa ambaye aliondolewa
mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Shekhe Ponda
alisomewa mashtaka ya uchochezi Agosti 14 mwaka huu akiwa kitandani katika
Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), akiwa chini ya ulinzi wa polisi tangu Agosti 9
mwaka huu, alipofikishwa hospitalini hapo kwa matibabu akitokea mkoani
Morogoro.
Kiongozi huyo
alifikishwa hospitalini hapo baada ya kudaiwa kupigwa risasi ambayo hata hivyo,
si MOI wala polisi waliothibitisha.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam, ililazimika kuhamia
hospitalini hapo kutokana na kulizwa Shekhe Ponda ambapo Bw, Kweka, alimsomea
mashtaka hospitalini hapo na kudai kuwa, Shekhe Ponda anatuhumiwa kufanya
uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini
alikana kutenda kosa hilo.
Majeraha na Majeruhi ya UKWELI ni anayajua asemaye na kuandika Urongo. Kama hvo Umezungumzwa Ukweli Ubeba wa UMETUMIKA,HVO mto hauvukwi.
ReplyDelete