Na
Mwandishi Wetu
WAZIRI M
kuuMizengoPind a,ame wataka Wa tanzaniakua cha tabia yakutemb eanapesamkonon ib
adalayake wa tumie mashinez akibenk i (ATM)katikakuhifadh i fedha zao kwa ajili
ya usalamawao.Hayo aliyaba inisha j anaji
jini Dar esSalamakatikahaf layauzind uz iwa hu dumaya Kadi mpyayaA TMyabenki
yaC RDBijulika nayok ama‘TemboCardChinaUnio nPay’ ,itakayotu mika bainayanc
hiyaChinan aTanzan iaili kuw e zaku rah isisha hu dumaza kibiashara katika nchi
hizo.
Pinda alisema kuwa kwa
kutumia mfumo wa kadi wa kibenki, utaweza kuzuia wezi kutumia nafasi ya kuiba
au kupora fedha kwa watu hasa wafanyabiashara pindi wabebapo fedha za biashara
mifukoni mwao."Naipongeza sana benki
ya CRDB kwa kuzindua huduma hii ambayo itawapa fursa wafanyabiashara wa
Tanzania na China kuweza kufanya biashara zao kwa umahiri na umakini na
kuwafanya wafanyabiashara hao kuhifadhi fedha mahali pa usalama ambapo sehemu
yoyote wahitajipo huduma ya fedha wanaweza kupata kwa urahisi," alisema
Pinda.
Alisema kuwa asilimia kubwa ya Watanzania bado
wanatabia ya kutembea na fedha mifukoni kwa lengo la kuonekana kuwa wana uwezo
wa kumiliki fedha nyingi, hali hiyo ni mbaya kwani inawafanya wezi kupata
nafasi ya kuiba kwa urahisi zaidi.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt.Charles
Kimei alisema kuwa benki ya CRDB imeweza kupanua wigo wake katika kuwafikia
wafanyabiashara wote wa nchi ya Tanzania na China, kwa kuwapa fursa ya
kuhifadhi fedha zao katika benki hiyo ambayo itawapa urahisi zaidi wa kufanya
shughuli zao za kibiashara wakati watakapohitaji huduma ya kifedha.
"Kadi ya China Union imejikita katika soko la
China ambayo ina uwezo wa kumrahisishia mteja kuingia katika mfumo wa malipo
ulio mzuri utakaowafanya wafanyabiashara wa Tanzania na wa China kufanya
shughuli zao kikamilifu bila woga wowote juu ya upotevu wa fedha," alisema
Kimei.Kimei alisema kuwa kadi hiyo
itaweza kuwawezesha wateja wa benki ya CRDB kufanya malipo yake akiwa nchini
China au Tanzania katika kufanya shughuli zake hasa za kibiashar
No comments:
Post a Comment