Na Mwandishi Wetu, Morogoro
KUFUATIAo
ng eze kokubwalawa gonjwawamoyokutokan ana ulajiwavyakula vin
avyotengenezwaviwandani, uo ngoziwaHospi tali yaM koawaMorogoro umetoa wi tokwa
jam ii nchinikutumiavy akulavya kiasili ili kuepukana naugonj wah uo
.Akizungu mzaM
ko aniMorogorowakati wahafla yakuk abidhiwa mashin eyauchu nguzi wamoy okutokaB
enk i yaKCBTanz ania, Ka imuMgangaMk uu waHosp italiyaRufa a Mkoa waMorog
oroDkt. RitaLyam uy a amesema , jamii ikijie pushanamatumizi yavyakulavya
kisasa idadi ya watu wanaopata matatizo ya moyo itapungua.
Akipokea msaada
huo, Dkt. Lyamuya alisema mashine hiyo ilikuwa ni moja ya hitaji lao kubwa
katika kukabiliana na ongezeko la wagonjwa waliokuwa wakihitaji huduma hiyo.Licha ya
kupatiwa mashine ya 'Cardiac Monitor' kutoka Benki ya KCB Tanzania bado
hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mashine za upasuaji
na vitanda vya akina mama kujifungulia.
"Tunaishukuru
Benki ya KCB Tanzania kwa kitendo cha kurudisha kiasi cha faida walichokipata
kwa jamii inayowazunguka kwa kutununulia mashine hii, tunaziomba taasisi
zingine zilizowekeza Morogoro kuiga mfano huu kwani kuchangia huduma za afya ni
kuboresha maisha ya jamii," alisema Dkt. Lyamuya.
Awali akikabidhi mashine hiyo, Meneja
wa KCB Tanzania tawi la Morogoro Hogla Laizer alisema, wamefikia uamuzi huo
baada ya kuona mahitaji ya wagonjwa wa moyo wanaofikishwa hospitalini hapo
kutoka mikoa ya jirani yakiongezeka.
Akifafanua Hogla alisema, licha ya
benki yake kuwahi kutoa msaada wa vitanda vya kujifungulia, mashine za upasuaji
na Oxygen, mashine ya joto kwa watoto njiti Warm Incubator ongezeko la watu
wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo liliwagusa na kuahidi kutoa msaada wa mashine
hiyo.
"Matatizo ya moyo yamekuwa
yakiongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi hiki cha Sayansi na Teknolojia,
msaada huu wa mashine ya kupimia moyo itasaidia kubaini mapema athari za
maambukizi kabla hazijawa kubwa na hivyo kupunguza idadi ya vifo kutokana na
ugonjwa huu," alisema Meneja huyo.
Hospitali zingine zilizofaidika na wiki ya Jamii
inayoendeshwa na Benki ya KCB Tanzania Mwananyamala, Temeke, Buguruni, Mount
Meru Arusha, KCMC Moshi na Mwembeladu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment