Na
Mwandishi Wetu
TAMASHA la Kili Music Tour,
linatarajiwa kuhamia jijini Mbeya ambapo Jumamosi hii, litafanyika katika
Uwanja wa New City Pub.Ta m a s h a h
i l o a m b a l o limeshafanyika katika baadhi ya mikoa, linatarajiwa kurindima
Mbeya kwa kushirikisha wasanii tisa wa muziki wa kizazi kipya pamoja na hip
hop.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George
Kavishe alisema tamasha hilo
linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maandalizi waliyoyafanya
.Alisema
maandalizi kwa kiasi kikubwa yameshafanyika, ambapo pia mashabiki wa muziki
mkoani humo watapata fursa kusikia nyimbo mpya za wasanii, watakaoshiriki
kwenye tamasha hilo.Aliwataja
wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha hilo kuwa ni Linex, Fid Q, Barnaba, Prof
J, Kala Jeremiah, Ben Paul, Izzo Biz, Snura pamoja na Awilo wa Mbeya.
"Tunashukuru
kuwa Watanzania wamepokea tamasha hili kwa moyo mkunjufu kabisa na walishiriki
kikamilifu kwenye mikoa ya Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Mwanza," alisema
Kavishe.Kavishe alisema lengo kubwa la tamasha
hilo ni katika kuondoa dhana ya Watanzania, kwamba kila kitu kinafanyika Dar es
Salaam, hivyo anategemea Mbeya itajumuika nao ipasavyo.
Kwa niaba ya wasanii wenzake msanii
mahiri wa muziki wa hip hop, Fareed Kubanda 'Fid Q' amewataka wakazi wa Mbeya
kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya New City Pub."Tumejiandaa vizuri kutoa burudani kali, ambapo mashabiki
watakaojitokeza watapata fursa ya kusikia baadhi ya nyimbo ikiwa ni pamoja na
zile mpya ambazo hawajawahi kuzisikia," alisema
No comments:
Post a Comment