WATU saba wamenusurika kifo baada ya
ndege ya kampuni ya Tanzanair kupata ajali na kuanguka ndani ya Ziwa Manyara
wakati ikitoka Bukoba kwenda Zanzibar,
anaripoti Grace Ndossa.Kamanda wa
Polisi mkoani Manyara, Akilimali Mpwapwa, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo
jana wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.
Alisema,ajali
hiyo ilitokea saa 8 mchana ambapo abiria wote waliokuwemo katika ndege hiyo,
waliokolewa ingawa rubani wake ambaye jina lake halikufahamika
mara moja alipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na uchunguzi
unaendelea.
Alisema
majeruhi hao waliokolewa kwa kutumia mi t umb w i p amo j a n a helikopta.Wakati huo huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametuma salamu za pole
kwa abiria hao na kuwapongeza walioshiriki kuwaokoa.
No comments:
Post a Comment