JOHN KIMBUTE
NI biashara ngapi ndogo zilizoansishwa na ni ngapi ambazo zimebaki
zinasonga mbele baada ya mwaka mmoja, miwili au mitatu? Jawabu siyo lazima liwe
jema au zuri kwa kila mojawapo kati ya juhudi hizo, hata katika nchi
zilizoendelea, Lakini inaelekea matatizo ya kuanzisha biashara, makampuni, huwa
ni mengi zaidi hapa. Hata hivyo inaelekea kuna fursa zinazoanza kujitokeza kwa
wingi zaidi hivi sasa, hasa kutokana na kukua kwa uchumi kwa asilimia saba (7%)
kwa mwaka.
Wachambuzi mara nyingine hawajui walie au wacheke wakisikia habari
za asilimia saba (7%) ya kukua kwa uchumi; wasiwasi huo ni sahihi kwani
haipunguzi umaskini. Ukuaji wa uchumi barani Afrika umesababisha kuzuka kwa makampuni
madogo kila upande, lakini mara nyingi kunakuwa hakuna aina mpya ya bidhaa
isipokuwa labda kwa mauzo ya maua
barani Ulaya na mazao kadhaa mapya ya kuuza nje. Mauzo ya nje ya viwanda siyo
nguvu halisi ya kiuchumi A f r i k a n a h a t
a mipango ya sasa hivi ya uwekezaji mkubwa kutoka Japan
na China bado haukidhi v i w a n g o v y a kuifanya
\Afrika inuke kikamilifu k a t i k a v i w a n d a .
Ingawainaweza kutoa kichocheo
cha Waafrika k u t e n g e n e z a b i d h a a kupunguza uagizaji. Kufikiria
kuanzisha kampuni au biashara fulani kunakanganyikiwa kuhusu maswali mawili; kama mtu ananzisha shughuli hiyo kwa vile anajua
kuifanya,au kwa sababu kuna hitaji kubwa sokoni la bidhaa au huduma anayotaka
kutoa. Ni vigumu kutambua kipi kinatangulia, kwani ni ukinzani mduara (tofauti
na ule ukinzani wa kuku na yai ambao ni wa chanzo na matokeo); hapa ni suala la
mfuatano,kuwepo sababu ya kutosha ya kuanzisha biashara fulani.
Siyo rahisi
kutoa jawabu la haraka kwa mfano kudai kama
bidhaa inahitajiwa, basi yeyote anaweza kuanza biashara hiyo. Inabidi kinachoanzishwa
kiwe ni mwendelezo wa kile ambacho tayari kipo, na kuzingatia hasa kupata
nafasi katika soko kwa ubora unaohitakiwa, bei, huduma yake, na muonekano. Kwa
maana hiyo, kila mtu anaweza kuanzisha kampuni kama
azima kuu sio fedha ila kuna jambo anataka kulifanya vyema na anaamini anaweza
kumudu. Inakuwa rahisi zaidi kuanzisha biashara inapokuwa inaendana na kile
unachopenda kufanya maishani, ni pale tu unapokuwa na shauku ya shughuli unayofanya
ndipo biashara yako inaweza kufanikiwa, Hapa biashara inakuwa ni zaidi ya pesa
kwani inakupa shauku na
maana ya maisha yako.
Mara nyingi inabidi
kuweka pembeni mahitaji binafsi na kutanguliza vipaumbele vya biashara kama vile kumudu ushindani unapoendesha soko. Hata hivyo
ni jambo lisilokwepeka kuwa biashara nyingi zinaanzishwa kwa nia ya kukwepa
mazingira yanayombana kwenye ajira, au hofu ya kupoteza ajiraau kutokujua hatma
yake punde atakapostaafu. Yapo makundi mawili ambayo yanaonekana zaidi katika
uanzishaji au uwepo wa makampuni na biashara nchini; wale ambao walirithi
biashara za familia , na ndiyo wanatawala kwa kiasi kikubwa zaidi mandhari ya
biashara au viwanda. Wako pia wale walioanzisha biashara kama
shughuli ya ziada wakiwa bado kazini, au wakijiandaa kustaafu. Wale wa kurithi huwa wafanyabiashara wanaofanikiwa kwa hulka yao,
wakati hawa wengine mafanikio yako mara nyingi hutegemea na
uzoefu wao na kama walianza mapema. Rais
Jakaya Kikwete aliwahi kuzungumzia suala hilo katika
hotuba mojawapo kitambo, wakati wa muhula wake wa kwanza, akizungumza kwa
ucheshi hasa kuhusu taarifa za kuanza biashara kadhaa tangu aingie Ikulu, pamoja
na suala zima la kutaja mali.
Alisema mtu asiingie katika biashara ambayo hadi anafikia umri wa miaka 35 bado
hajaanza kuifanya, kwa maana kuwa biashara ya aina fulani (siyo biashara tu ili
kutafuta fedha na kuganga njaa) ni kitu mtu anakuwa nacho kuanzia ujana halafu wakati
fulani anakuwa na nafasi ya kuanza kukifanyia kazi. Ndiyo maana umri huo wa miaka 35,
kwa mtu mwenye nia halisi ya mwelekeo fulani, labda atakuwa tayari ameanza kujipanga
. Hata hivyo
inawezekana kuchelewa na bado ukafaulu, kama kile unachofanya ni kitu kimekuwepo
kichwani kinaendelea kuchambuliwa kwa muda mrefu, siyo kimezuka tu ghafla bin
vu kama “ndoto za Alinacha.” Wazo linapokuwa
kimeshaanza kufanyiwa kazi kwa miaka mingi, yakitokea matatizo na majawabu
yanakuwepo,lakini wakati ambapo kama ni biashara imezuka tu,ujuzi na umahiri wa
kutegua mitego na matatizo pia unakuwa mdogo.Msingi na maandalizi mazuri
huishiria hatma ya biashara inayoanzishwa.
Mbali na hapo, kwa kutumainia tu
njia za mkato ni rahisi kupotea njia na kujikuta kwenye
majuto kama
sio kuhangaika na kutumia fedha kutafuta ushauri, wakati ambapo hakuna mshauri
anaweza
kuchukua nafasi ya hisia na utashi.Mazingira ya ajira hutegemeana na aina ya mfanyakazi anayetafutwa. Kwa mfano, mwajiri atafanikiwa
zaidi kama kampuni yake inatoa fursa za
kuwaendeleza wafanyakazi. Hiki ni kivutio kwa wafanyakazi wa kati tofauti na
walewaliokwisha fikia ngazi za juu.
Kukuza
No comments:
Post a Comment