22 August 2013

FAMILIA YAMBURUTA LIYUMBA KORTINI



Na Rehema Maigala

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala na Fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, amefunguliwa kesi ya madai na mke wake, Aurelia Ngowi, akiiomba mahakama hiyo imzuie aache kutawanya mali za familia ikiwa ni pamoja na kutaka kuuza nyumba anayoishi na watoto
.Kesi hiyo ya madai imefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni na mke wake ambaye anadai kufunga ndoa ya kimila na Liyumba, mwaka 1978 mkoani Kilimanjaro.Kesi hiyo ya madai ilitajwa mahakamani hapo jana na kisha kuahirishwa hadi kesho ambapo mahakama itatoa uamuzi kuhusiana na pingamizi lililowasilishwa mahakamani na mdaiwa (Liyumba).
Mlalamikaji anaitaka mahakama itoe amri ya kumzuia mdaiwa asitawanye mali za familia hadi kesi ya msingi itakapomalizika.Mbali na madai hayo, mlalamika ameiomba Mahakama imruhusu yeye na watoto wake waendelee kuishi katika nyumba hiyo ambayo anadai tayari amefukuzwa na mume wake (Liyumba) tangu mwaka 1980.

Kesi hiyo ya madai ipo mbele ya Hakimu Jackline Rugemalila, ambapo mlalamikaji anatetewa Margaret Ringo.Hata hivyo, mdai aliwasilisha kiapo chake Mahakamani,ambacho kilieleza kuwa alifunga ndoa na mdaiwa mwaka 1978 Kilimanjaro na kufanikiwa kupata watoto wanne ambao ni, Lyinda Liyumba, Jennifer Liyumba, Priscus Liyumba na Yulia Liyumba.

Katika kiapo hicho anaeleza kuwa walikuwa wanaishi katika nyumba hiyo iliyopo Mbezi Beach maeneo ya Afrikana kitalu No.2232/2233.Kiapo hicho kinaeleza kuwa mdaiwa baada ya kutoka gerezani mwaka 2012, alirudi nyumbani kwake na kuuza magari mawili,aina ya Range Rover, Land Cruiser, Trekta, Benzi, Jenereta na shamba lenye ekari 50 ambalo lipo Bagamoyo mkoani Pwani na ploti nyingine iliyopo Tabata. Alidai kuwa mali hizo zote zilikuwa ni mali ya familia.

1 comment:

  1. hii story binafsi sijui kama inaukweli ndani yake kwani liyumba kila alioaga mwanamke mmoja tu maishani mwake na ndiye alitambulika na serikali na kila mtu ambae kwa sasa ameshafariki na huyo mama sio huyu mchaga ywye alikuwa kama amechanganya na uzungu na aliachaga mtoto mmoja tu. huyu mana ngowi alizaaga nae tu miaka zaidi ya 30 ilopita. na liyumba kazaazaa tu na wanawake wengi tofauti na kwa ujumla anawatoto kama 10. watu wengine wanataka tu umaarufu kupitia magazeti!.

    ReplyDelete