Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Bi. Beatrice Mallya (kushoto), akimkabidhi funguo ya nyumba iliyopo Kibada Dar es Salaam, mkazi wa Iringa, Bw. Silvanus Juma, ambaye ni mshindi wa shindano la 'Shinda Nyumba na Airtel Yatosha'. wakati wa hafla iliyofanyika Kibada jana
Na Frank Monyo
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel
imemkabidhi mshindi wa nyumba mkazi wa Iringa, Bw. Silvanus Juma, nyumba ya
kisasa ya vyumba vitatu yenye thamani ya sh.milioni 65 baada ya kuibuka mshindi
katika droo ya kwanza ya mwezi ya promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba
.Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano ya nyumba hiyo jana Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa mawasiliano Airtel, Beatrice Mallya, alisema nyumba hiyo imegharimu sh.
milioni 65.
Alisema kuwa lengo ni kutoa maisha bora
kwa Watanzania kupitia katika shindano la shinda nyumba na Airtel Yatosha."Mshindi amejinyakulia nyumba ya
kisasa ya vyumba vitatu iliyopo Kigamboni Kibada kwa kushiriki kwenye
promosheni ya Airtel yatosha na kununua vifurushi," alisema.
Alisema kuwa zimebaki nyumba mbili
ambapo kila mwisho wa mwezi watatoa mshindi wa nyumba kupitia katika promosheni
hiyo ambapo jinsi ya kushiriki ni kupiga *149*99# kisha anajiunga kwenye
vifurushi vya Airtel yatosha
Naye mshindi wa nyumba Bw.Juma alisema
amefurahi sana kwa kushinda zawadi ya nyumba kutoka Airtel kwani imembadilisha
maisha yake."Hili shindano ni la kweli hakuna upendeleo
wala ubaguzi hivyo ninawasihi Watanzania wenzangu ambao ni watumiaji wa Airtel
kushiriki katika shindano hili," alisema
No comments:
Post a Comment