MWANDISHI
Gladness Theonest
‘‘
Hapo baadaye itabidi tutumie teknolojia ambayo itaweza
kuondoa sumu iliyopo ziwani kwani itakuwa ni nyingi hivyo wananchi itabidi
watumie maji ya visima
PAMOJA n a j u h u d i
zinazofanywa na miradi mbalimbali ya mazingira ya kuhakikisha Ziwa Victoria
linakuwa salama, bado harakati hizo zimegonga mwamba kutokana na uchafu ambao
umekuwa ukitupwa ziwani
. Hatua hiyo inaonesha kuwa, idadi ya watu wanaolitunza ziwa hilo ni
ndogo kuliko wanaochafua mazingira. Baadhi ya watu waishio maeneo yanayozunguka
ziwa hilo zikiwemo taasisi, hoteli na viwanda, hutupa uchafu mwingi ziwani.
Kutokana na hali hiyo, hivi sasa madhara mbalimbali yameanza
kujitokeza kwa binadamu na viumbe hai vilivyomo ziwani. Madhara hayo ni pamoja
na mlipuko wa magonjwa kwa binadamu na vifo. Pia kuna sumu nyingi ziwani, kina
cha maji na samaki kupungua, kufa na ubora wa maji kubadilika.
MKEMIA AZUNGUMZA
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kaimu Meneja wa Maabara
ya Ubora wa Maji mkoani Mwanza, Novat Kessy ambaye anasema, pamoja na maji ya
ziwa hilo kuendelea kutumika, bado uchafuzi mkubwa unaendelea kufanyika.
Anasema katika ziwa hilo kuna uchafu wa vinyesi vya binadamu na
kemikali zinazomwagwa na viwanda vilivyopo jirani na ziwa hivyo kusababisha
uwepo wa virutubisho vingi katika maji ambavyo vimechangia kuwepo kwa mimea
kwenye maji ijulikanayo kwa jina la kitaalamu "Phytoplankton"
Mimea hiyo ambayo ni midogo, imegawanyika katika makundi mawili,
iko yenye rangi ya kijani ambayo ni chakula cha samaki yaani (Phytoplankton
Green) na rangi ya bluu ambayo ni sumu kwa samaki (Phytoplankton Blue).
HATARI ILIYOPO
Kessy ambaye ni Mkemia, anasema kutokana na sumu ambazo
zinaendelea kuzalishwa ziwani kutokana na virutubisho hivyo, teknolojia
inayotumika sasa kutibu maji (water treatment ), haitakuwa na uwezo wa kutibu
maji hayo kutokana na uwepo wa vijidudu vingi (sumu), ziwani.
"Tatizo kubwa ambalo linachangia maji yashindwe kutibiwa hapo
baadaye ni wingi wa vijidudu vya Phytoplankton, hivi sasa teknolojia
inayotumika ni ile ya kuondoa tope na kutibu maji ili kuondoa vijidudu
vinavyosababisha magonjwa ya milipuko.
"Hapo baadaye itabidi tutumie teknolojia ambayo itaweza
kuondoa sumu iliyopo ziwani kwani itakuwa ni nyingi hivyo wananchi itabidi
watumie maji ya visima," anasema.
MADHARA YA SUMU
Kutokana na wingi wa sumu hiyo ziwani, Kessy anasema hali hiyo
inachangia viumbe hai kama samaki waliopo ziwani washindwe kuishi kutokana na
mimea hiyo kusababisha hewa ya oksijeni kukosekana katika maji.
Anasema ifikapo Machi
kila mwaka, samaki wakubwa hufa kwa kukosa oksijeni ambapo kipindi hicho maji
huwa yanajichanganya.
"Ile mimea yenye
virutubisho inakuwa inaoza kwa sababu ya kuozeshwa na wadudu, baaadaye
inakwenda chini na kusababisha bakteria wanaotumia oksijeni...hali hii
huchangia oksijeni kupungua ziwani na samaki kufa," anasema Kessy.
Anaongeza kuwa,
madhara mengine yanarudi kwa jamii kwani awali gharama ya maji ilikuwa ndogo
lakini kutokana na pesa nyingi inayotumika kutibu maji, bili za maji kwa
wananchi zitalazimika kupanda kila mwezi.
MAA BARA YA MA
J I BUKOBA
Mkuu wa Maabara hiyo,
Marco Vita anasema ubora wa maji katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera,
wakati wa masika unakuwa mbaya zaidi kutokana na watu kutumia mwanya huo
kutapisha vinyesi na kulifanya ziwa hilo kuwa chafu.
Anasema kutokana na
hali hiyo, wanalazimika kutumia dawa nyingi ya kutibu maji licha ya Mamlaka ya
Maji safi na Maji taka Bukoba (BUWASA), kuweka dawa ya kutibu maji kabla
hayajaenda kwa wananchi kwa ajili ya matumizi.
"Dozi wanayoweka
BUWASA bado haitoshelezi kutokana na maji hayo kuonekana machafu...hivi sasa
magonjwa ya kuharisha, matumbo kwa watoto na watu wazima, yanaongezeka kwa kasi
kubwa ambapo wananchi pia hulazimika kuchemsha maji," anasema.
WADAU WA
MAZINGIRA BUKOBA
Bw. Michael Cleophans
ni mdau wa mazingira na Katibu Mkuu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya
Envirocomet ambaye anadai kuwa, uchafuzi wa mazingira katika ziwa hilo umeleta
madhara mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba na maeneo mengineyo.
Anasema kumekuwa na
bakteria wengi kwenye samaki ambao huathiri watumiaji samaki na watu
wanaokwenda ziwani kuoga kupata magonjwa ya ngozi.
"Vyanzo vingi
vya maji vimeendelea kukauka, ukilinganisha na miaka 10 iliyopita, kina cha
maji katika ziwa hili kimepungua kwa mita mbili... hivi sasa ziwa limebaki na
aina tatu tu za samaki ambao ni sato, sangara na dagaa.
"Pamoja na
kuwepo kwa samaki hawa, pia wingi wao umepungua ziwani ambapo kipindi cha miaka
10 iliyopita, zilikuwa zinavuliwa tani 750 za samaki lakini kwa sasa zinavuliwa
tani 350 tu.
Bw. Cleophans
anasema, uvuvi haramu umekuwa mkubwa kuliko utunzaji wa ziwa na samaki ambapo
taka ngumu zimekuwa zikimwagwa ziwani na kuwa chakula cha samaki.
WANANCHI WA
KAWAIDA
Bw. Thomas Ngaiza
ambaye ni mkazi wa Mji wa Bukoba, anasema kutokana na uchafu wa mazingira
uliopo katika ziwa hilo, hivi sasa kuna magonjwa mengi ya milipuko hospitalini
ukiwemo wa tumbo (typhod), ambayo awali hayakuwepo.
Anasema maji
yanayotumiwa na wananchi majumbani ambayo hutibiwa na BUWASA yamekuwa machafu
sana pamoja na ongezeko la magonjwa ya ngozi.
KAIMU MGANGA
MKUU
Kaimu Mganga Mkuu wa
Manispaa ya Bukoba, Dkt. Martin Muganyizi, alipohojiwa kuhusu magonjwa yatokanayo
na matumizi ya maji ya ziwa hilo kwa wananchi, alisema kwa sasa yamekuwa mengi.
Anasema mwaka
2011/2013, magonjwa yaliyoripotiwa ni pamoja na kuhara, homa za matumbo ambayo
ilionekana kuwashambulia watu wengi zaidi kutokana na matumizi ya maji hayo na
magonjwa ya ngozi.
Anaongeza kuwa, kundi
ambalo linaathirika zaidi kutokana na magonjwa hayo ni watoto na wazee ambao
uharisha ambapo vijana na wazee pia huathirika zaidi na magonjwa ya ngozi.
TAKWIMU ZA
MAGONJWA
Dkt. Muganyizi
anasema, katika kipindi cha mwaka 2011-13, jumla ya kesi 12,556 za magonjwa ya
kuharisha zilizolipotiwa zikijumuisha watoto walio chini ya miaka mitano na
zaidi.
"Wanaume
walikuwa 5,708, wanawake 6,848, katika magonjwa ya ngozi kulikuwa na kesi 4,643
ambazo ziliripotiwa katika kipindi hicho wakiwemo wanaume 2,399, wanawake
2,244," anasema.
VIFO
VILIVYOTOKEA
Dkt. Muganyizi
anasema, vifo vilivyoripotiwa katika kipindi cha mwaka 2011-12 kwa ugonjwa wa
kuharisha pekee wagonjwa 42 walipoteza maisha (chini ya miaka mitano na zaidi),
kati ya hao, wanaume 29, wanawake 13.
JAMII IFANYE
NINI
Ili kuepuka vifo na
madhara mengine yatokanayo na matumizi ya maji katika ziwa hilo, Dkt. Muganyizi
anasema jamii inapaswa kunywa maji yaliyo safi na salama yaliyochemshwa na
kutibiwa, matumizi sahihi ya vyoo, kuosha matunda kabla ya kula, kunawa mikono
kwa maji safi na sabuni kabla ya kula, kutoka chooni.
Aliitaka BUWASA
iboreshe huduma za usambazaji maji safi kwa wananchi na kuishauri jamii,
viwanda, hoteli na taasisi kuhakikisha shughuli zao hazichafui mazingira ya
ziwa hilo ambalo lina msaada na mchango mkubwa kwa wananchi na Taifa.
U t a f i t i wa makala h i i
umefadhiliwa na Mfuko wa Vyombo vya Habari nchini (TMF).
No comments:
Post a Comment