Na David
John
BARAZA Kuu la Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu nchini, limesema kipengele cha uwepo wa Mahakama ya Kadhi kwenye
Katiba Mpya, hakiepukiki hivyo ni wajibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
kuhakikisha Waislamu wanapata haki yao
ya msingi.
Mwenyekiti
wa baraza hilo, Shekhe Mussa Yusufu Kundecha, aliyasema hayo Dar es Salaam jana
katika mkutano waliouitisha ili kupitia Rasimu ya Katiba Mpya ulioshirikisha
wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Alisema Mahakama ya
Kadhi ni jambo muhimu kwa Waislamu hasa katika eneo la mirathi na mambo mengine
ambapo awali waliwasilisha ombi hilo kwa Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu
Joseph Warioba kabla rasimu hiyo haijatoka.
"Tu l i p e n d
e k e z a k uwe p o kipengele cha kuitambua mahakama hii kwenye Katiba Mpya
lakini kinyume na hapo, tume imekataa mapendekezo yetu...tunatarajia kuyapeleka
tena kwa tume husika ili katiba iweze kuleta matumaini ya Watanzania
wote," alisema.
Naye mjumbe wa baraza
hilo kutoka Temeke, Dar es Salaam, Shekhe Abubakar Shabani alisema,
watahakikisha suala hilo linapigiwa kelele ili liweze kuingizwa katika Katiba
Mpya.
Alisema hata ombi lao
la kutaka siku ya Ijumaa iwe mapumziko pia limekataliwa na tume hiyo kama
ilivyo Jumapili kwa Wakristo hivyo ni wazi kuwa Waislamu hawatendewi haki.
"Ijumaa ni siku
ya ibada kwa Waislamu hivyo inastahili iwe ya mapumziko kama ilivyo Jumamosi na
Jumapili, kama haiwezekani Serikali ichague siku nyingine ya mapumziko ambayo
itakuwa inatendeka haki kwa pande zote," alisema Shekhe Shabani.
Aliongeza kuwa, pendekezo lingine ambalo walilipeleka kwa
tume hiyo ni kuruhusiwa kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC),
lakini imekataa mbali ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. Benard Membe kusema suala hilo
halina tatizo lolote kwa Waislamu.
BASI TUME IJIAMULIE YENYEWE WATU WASITOE MAPENDEKEZO YAO. AU WANAFANYA HIVYO KWA WAISLAM TU?
ReplyDeleteBORA TUME IKATAE MANAKE MWISHO WA SIKU MKIKUBALIWA MNAKUAGA TATIZO KWELI..HAPA MAHAKAMA YA KADHI HAIJAKUBALIWA MPO BIZE KUCHOMA MAKANISA JE IKIKUBALIKA ITAKUAJE?ALAFU MNADAI MNAONEWA SIWAELEWI HATA KIDOGO CJUI MNATAKA NINI.
ReplyDeleteNITAJIE MUISLAM AMBAYE KACHOMA KANISA.
DeleteSIWEZI KUTAJA KWA SABABU HAPA SI ENEO LA KUSHTAKI MTU.NA KAMA SI MUISLAMU NANI KACHOMA AU UNATAKA KUSEMA WAKRISTO WENYEWE NDO WAMECHOMA MAKANISA?BASI MPAGANI NDO KACHOMA LOL!
DeleteHIVI JAMANI WENZUTU KAMA MNATAKA MAHAKAMA YA KADHI KWA NINI MSIIPITISHE HUKO KWENYE JUMUIYA ZENU BADALA YA KUNG'ANG'ANA LIWE JAMBO LA KITAIFA?HAMUONI KAMA MNALETA UDINI KATIKA TAIFA LETU?ACHENI UDIKTETA.
ReplyDeleteMbona BAKWATA hamuitaki kwa kusema kuwa imeanzishwa na serikali? Inakuwaje tena mnaitaka serikali hiyo hiyo ianzishe Mahakama ya Kadhi? Double standards!
ReplyDeleteMungu wetu asimame katika hili, hawa wenzetu wanaleta shida sana sijui ni mbingu gani wataingia hawa jamaa, mi cwaelewi kabisa, E MUNGU TUNUSURU KATIKA HILI,
DeleteHATA KIDOGO WEWE SI MUELEWA.TOFAUTISHA KUANZISHWA NA KUWEKWA KWENYE KATIBA.HAYA NI MAONI LAZIMA YAFANYIWE KAZI
Deletena nyie bwana mmezidi sasa mnataka watu wasifanye kazi ijumaa...kwa hyo siku za kazi ziwe nne tu.maendeleo yatatoka wapi?
ReplyDelete