22 August 2013

MALIPO YA WALIOSHIRIKI SENSA YAIVA



Na Jovither Kaijage, Ukerewe
OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, jijini Mwanza imepokea sh. Milioni 25 kwa ajili ya kulipa posho za wenyeviti wa vitongoji walioshiriki Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ukerewe, Godwin Mlosso, aliyasema hayo katika kikao cha Wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa kata
tatu za Mriti, Mukituntu na Bukongo jana ambapo alisema zinaitajika sh. milioni 29 kwa ajili ya malipo hayo.

Alisema taratibu zinafanyika ili kurejesha sh. milioni 4 ili zilizorejeshwa hazina ndogo ijini Mwanza baada ya baadhi kukataliwa na wenyeviti wa vitongoji wakipinga malipo ya awali ya kila mmoja kulipwa sh. 14,000.
Alifafanua kuwa baada ya serikali kukubaliana nao kuwalipa sh. 70,000 kila mmoja ndipo zimeongezwa fedha nyingine. Aliongeza kuwa katika malipo hayo baadhi yao watalipwa sh. 56,000 kwa sababu awali
walilipwa sh. 14,000. Mlosso alitoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za viongozi hao wa ngazi ya vijiji na
vitongoji waliotaka Serikali iwaeleze ukweli juu ya madai yao. Akizungumza katika kikao hicho kilichoandaliwa na Shirika la Mzeituni Foundation na kuhudhuriwa na wajumbe 102 wakiwemo baadhi ya watendaji wa
kata na vijiji, Mlosso aliwataka viongozi hao wa vijiji na vitongoji katika wilaya hiyo kuwa na uvumilivu kwa sababu yatalipwa hivi karibuni.Naye Mkurugenzi Mzeituni Foundation, Meshaki Masanja, aliwataka viongozi hao kurejesha moyo wa kazi ili kuepuka kukata tamaa.

No comments:

Post a Comment