Na Mariam Mziwanda
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC), imesema aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mvomero, mkoani Morogoro, Bi. Sarah Linuma na Mweka Hazina wake, Bw. Stima
Kabikike, wanapaswa kutafutwa ili waweze kujibu tuhuma ya hesabu hewa sh.
bilioni 1.2 za halmashauri hiyo.
Makamu
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Selemani Zedi, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika kikao chao na
kusisitiza kuwa, pamoja na Bi. Linuma kuomba kustaafu na Bw. Kabikike kuhamishiwa
Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam,
ukweli utabainika juu ya matumizi hewa ya fedha hizo za umma.Alisema ripoti
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini matumizi ya
fedha hizo hayajathibitishwa na haijulikani zimefanyia kitu gani.
“Tunafanya
taratibu za kumsaka Bi. Linuma ambaye ameomba kustaafu na Bw. Kabikike waje
kutuambia kwanini matumizi ya sh. bilioni 1.2 hazina nyaraka kwa CAG na
haijulikani zipo wapi.“Pia kamati hii
imebaini katika halmashauri hiyo, kuna ujenzi wa ofisi hewa ya Mkurugenzi
kutokana na CAG kutokuwa na taarifa ya malipo sh. milioni 39 alizolipwa
mkandarasi ambazo ni zaidi ya fedha zilizoainishwa katika mkataba,” alisema.
Aliongeza kuwa, kumekuwa na ubadhirifu
katika ulipaji malipo ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi hivyo kuitaka
halmashauri hiyo kuhakikisha fedha zote zinapelekwa ili wafanyakazi hao
wanapofikia umri wa kustaafu waweze kupata viinua mgongo vyao.Kamati hiyo iliiagiza halmashauri hiyo
kupeleka zaidi ya sh. milioni 94 za miradi ya vijijini ambazo hazikufikishwa na
uhakiki ufanyike ili fedha halali zijulikane na kupelekwa kabla mwaka huu wa
fedha haujamalizika.
Akizunguzia matumizi hewa ya fedha za
miradi ya wanawake na watoto katika halmashauri hiyo, Bw. Zedi alisema ni
kinyume na sheria kutumia fedha hizo katika matumizi mengine.
Matumizi hayo ni pamoja na kulipana posho na kuitaka h a l m a s h a u r
i k u h a k i k i s h a watakapokutana tena na kamati hiyo wawe na ripoti
inayoonesha uwezo wa kujitegemea kwa asilimia 10 na kuamuru malipo yote sasa
kufanyika kwa mashine za elektroniki
No comments:
Post a Comment