23 August 2013

CCM KUJADILI MAONI RASIMU KATIBA MPYA



 KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, inatarajiwa kukutana leo Mjini Dodoma ambapo kikao hicho kitafuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu Agosti 29 mwaka huu ambacho kitakaa kwa siku mbili mfululizo, anaripoti Elizabeth Joseph, Dodoma
.Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Bw. Nape Nnauye, alisema ajenda Kuu ya Kamati Kuu ni kujadili maoni ya wanachama wa chama hicho kuhusu Rasimu ya Katiba.
Bw. Nnauye alisema, hadi sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria, taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Pia kikao cha kesho (leo), kitajadili hali ya kisiasa, hatma ya madiwani Mjini Bukoba, mkoani Mara na masuala ya utumishi ambapo kesho, kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri.
“Baraza hili linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa,” alisema Bw. Nnauye.
Katika hatua nyingine, Bw. Nnauye alisema mikutano ya hadhara inayoendelea kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kukusanya maoni ya Katiba Mpya ni ushamba wa kutojua sheria za siasa.
Bw. Nnauye aliyasema hayo Mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa ni ushamba kuwaita wananchi hadharani ili kujadili Rasimu ya Katiba jambo ambalo linawachosha.
“CHADEMA badala ya kuandaa Mabaraza ya Katiba, wao wanafanya mikutano ya hadhara huu ni ushamba mkubwa wa kutojua sheria.
“Tunamshukuru Jaji mstaafu Joseph Warioba ambaye amesema hatapokea maoni ya wazi kama walivyofanya CHADEMA... CCM iko tofauti kwani tumeita wanachama na kujadili rasimu hii na maoni yaliyotolewa yatapitiwa kwenye kikao cha Kamati Kuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.
Aliongeza kuwa, baada ya vikao hivyo kupitia maoni hayo, yatawekwa pamoja na kuwasilishwa katika Tume ya Katiba.
“Sisi tunaonesha mfano kwa kuyawasilisha maoni ya wanachama wetu katika vikao vya Kamati na Halmashauri Kuu ambavyo vitafanyika leo na kesho hapa Dodoma,” alisema

4 comments:

  1. CCM ni chama kikongwe na kikubwa. Hata hivyo changamoto iliyopo ni uhamasishaji wa wanachama waliopo na kushawishi wapya. CHADEMA isidharauliwe tusije umumbuka.

    ReplyDelete
  2. Sioni kama ni busara kwa nchi inayosifiwa kwenye uso wa dunia kuwa ya kistarabu kuandikia habari kama vile ambavyo zimeandikwa "ushamba"

    tujifunze kutumia tafsida kama njia ya kupunguza ukali wa maneno ilimradi ujumbe uwafikie walengwa au jamii husika.

    ReplyDelete
  3. Bw. Nnauye, anachekesha sana. Hivi kwa nini ana hurka ya kukurupuka kiasi hicho? Analewa madaraka kama mugabe na kuona as if wengine hawajui au hawamjui! alipotaka kuanzisha CCJ akiwa na kundi lake lengo lilikuwa nini,

    Sasa eti ccm mkoa kagera unawavua uanachama madiwani feki wanaokwamisha maendeleo na ghafla anatoa agizo kuwa hatambui uvuliwaji huo, hivi huyo ni kihio mwingine au vipi. Nnape bora uungane na madiwani nane mkaanzishe chama chenu kuliko kukikoroga chama chetu.

    ReplyDelete
  4. Swala la urai wa nchimbi sio swala la chama Fulani cha kisiasa. Ni swala la Watanzaia wote. wapo wanao lipinga na wana-oliunga mkono regardless of their vyama vya kisiasa. Nisilo lipenda ni kwa wanasiasa wanafki kuliushisha swala hili ni chama Fulani cha kisiasa na kuwatisha wananchi. Ukitizama nchi zilizo ruhusu uraia wa nchi mbili,mfano Kenya,uganda,Burundi South Africa & etc.Nchi hizo hazijawahi kuingia kwenye matatizo ya kisiasa/kiusalama eti kwa sababu zina toa duo-citizenship. Hapa bongo watu watakao faidika na duo citizenship wengi wao ni watazania wenzetu and most of them have clean money sio hizo pesa za kifisadi/unga za wanasiasa wa hapa bongo.
    Enzi za Baba Wataifa "MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE", TZ haikuitaji kuwa na duo-citizenship kwa sababu tulikuwa na wa TZ wacheche sana walio uhitaji. Tutakuwa wanafki tukisema bado hatu-huitaji wakati kuna zaidi ya wabongo 2million wanaoishi abroad.
    Shukrani.

    ReplyDelete